Msanii Kid Cudi Aoa Mpenzi Wake wa Muda Mrefu Nchini Ufaransa

Msanii Kid Cudi Aoa Mpenzi Wake wa Muda Mrefu Nchini Ufaransa

Msanii maarufu wa muziki wa Rap na muigizaji mashuhuri, Kid Cudi, ametangaza rasmi kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu, Lola Abecassis Sartore, ambaye sasa anafahamika kwa jina jipya la ndoa, Lola Mescudi. Ndoa hiyo ya kifahari ilifungwa tarehe 28 Juni 2025 katika eneo la kifahari la Cap Estel, lililopo katika mji wa Èze, kusini mwa Ufaransa. Sherehe hiyo ilifanyika kwenye bustani ya kuvutia inayotazama moja kwa moja Bahari ya Mediterania, ikihudhuriwa na ndugu wa karibu, marafiki wa familia na wageni maalum kutoka tasnia ya burudani. Kid Cudi, ambaye jina lake halisi ni Scott Mescudi, ameweka wazi furaha yake kupitia mitandao ya kijamii, akionesha picha chache kutoka katika tukio hilo la kipekee, huku mashabiki na watu maarufu wakimpongeza kwa hatua hiyo muhimu ya maisha. Ndoa hii inakuja wakati ambapo Kid Cudi ameendelea kuimarika kitaaluma, akiwa na mafanikio makubwa katika muziki, uigizaji na hata ubunifu wa mitindo.

Read More
 Ushahidi wa Kid Cudi Dhidi ya Diddy Wamvunja Moyo Kanye West

Ushahidi wa Kid Cudi Dhidi ya Diddy Wamvunja Moyo Kanye West

Rapa maarufu mwenye utata, Kanye West, ametoa hisia zake kuhusu hali inayoendelea kumkumba Sean Diddy Combs, akieleza masikitiko yake juu ya hatua ya Kid Cudi kutoa ushahidi dhidi ya Diddy. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Ye ameonekana kuzungumzia kile anachokiona kama mfumo wa haki unaowakandamiza watu weusi, akisisitiza haja ya jamii ya wasanii na Wamarekani Weusi kwa ujumla kujilinda na kushikamana badala ya kushirikiana na mifumo anayoamini kuwa ya kibaguzi. “I wish Cudi hadn’t testified against Puff. We need to not be locked in white systems. Praying for Puff and his family. Praying for Puff Daddy and the Family.”Aliandika X Kauli hiyo imeibua hisia mseto kutoka kwa mashabiki na wanamuziki wenzake, huku baadhi wakimtetea kwa msimamo wake wa kutaka mshikamano miongoni mwa wasanii wa asili ya Kiafrika, na wengine wakimkosoa kwa kudharau mchakato wa haki. Kid Cudi, ambaye zamani alikuwa rafiki wa karibu wa Ye, anatajwa kuwa miongoni mwa mashahidi waliotoa ushahidi dhidi ya Diddy kufuatia madai mazito yanayomkabili kuhusu vitendo vya unyanyasaji na ukiukaji wa haki.

Read More
 Young Thug Amshambulia Kid Cudi kwa Madai ya Kutoa Ushahidi Dhidi ya Diddy

Young Thug Amshambulia Kid Cudi kwa Madai ya Kutoa Ushahidi Dhidi ya Diddy

Mastaa wawili wa muziki wa hip hop, Young Thug na Kid Cudi, wameingia kwenye mzozo wa wazi baada ya Cudi kuonekana mahakamani kutoa ushahidi unaomkabili rapa nguli Sean “Diddy” Combs, katika kesi inayohusisha tuhuma za unyanyasaji, ukatili na matumizi mabaya ya madaraka. Kupitia chapisho aliloliweka kwenye akaunti yake ya X (zamani Twitter), Young Thug aliandika neno “rat” huku akimtag Kid Cudi, kauli ambayo katika muktadha wa mitaani na muziki wa hip hop humaanisha msaliti au mtu anayewasaliti wenzake kwa kushirikiana na vyombo vya sheria. Ingawa Thug alifuta chapisho hilo muda mfupi baadaye, tayari liliwasha moto mitandaoni, huku mashabiki wakitofautiana kuhusu uhalali wa hatua hiyo. Kid Cudi alionekana kizimbani mwishoni wiki jana kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili Diddy, msanii na mfanyabiashara mwenye ushawishi mkubwa katika tasnia ya muziki wa Marekani. Taarifa zinasema ushahidi wa Cudi unahusiana na matukio ya zamani ambayo huenda yakawa na uzito mkubwa katika uamuzi wa mwisho wa kesi hiyo. Young Thug, ambaye kwa sasa naye anakabiliwa na kesi kubwa ya RICO (Racketeer Influenced and Corrupt Organizations Act) inayohusisha mashitaka ya uhalifu wa genge, ameonekana kuchukulia hatua ya Cudi kama ukiukaji wa kanuni za mtaa, zinazokataza kushirikiana na mamlaka au kutoa ushahidi dhidi ya wenzako. Wachambuzi wa masuala ya burudani wanasema huenda Thug anaangalia hali hiyo kwa jicho la mtu anayepitia mchakato wa kisheria na kuona kwamba hatua kama ya Cudi zinaweza kudhuru watu walioko kwenye mazingira kama yake. Kauli ya Thug imezua mijadala mikubwa, huku upande mmoja wa mashabiki ukimtetea Kid Cudi kwa kusema kwamba hatua yake ni ya kijasiri na inalenga kusaidia kutendeka kwa haki. Wengine wanasema Cudi amevunja misingi ya mshikamano katika jamii ya hip hop kwa “kuwageuka” wenzake. Mpaka sasa, Kid Cudi hajajibu moja kwa moja tuhuma au kejeli hizo kutoka kwa Young Thug. Vyanzo vya karibu na msanii huyo vinaeleza kuwa ameweka mkazo kwenye ukweli na kutafuta haki kwa waathirika.

Read More
 Kid Cudi atangaza kustaafu muziki

Kid Cudi atangaza kustaafu muziki

Rapa kutoka Marekani Kid Cudi ametangaza kuwa anafikiria kuachana na Muziki baada ya kuachia Album yake mpya ‘Enterlagactic’ ambayo ilitoka September 30 mwaka huu. Kwenye mahojiano na Zane Lowe wa Apple Music Beats 1, Kid Cudi amesema anafikiria kuupa muziki kisogo. Sababu kubwa ambayo aliitaja Kid Cudi ni kuwa amechoka kuachia Album na kutengeneza Muziki, huku akieleza kwamba anataka kujitupa kwenye fani nyingine ya kuandaa maudhui ya Televisheni na kuandika filamu.

Read More