Cheed na Killy wafuta urafiki na Harmonize Instagram

Cheed na Killy wafuta urafiki na Harmonize Instagram

Wasanii Cheed na Killy huenda kwa sasa wakawa hawataki kuona chochote kuhusu Harmonize. Wawili hao wameamua kumu-unfollow bosi wao huyo wa zamani katika kurasa zao za Instagram baada ya lebo ya Konde Music Worldwide kusitisha mkataba wao kwa sababu ambazo hawakuziweka wazi. Utakumbuka mwisho mwa wiki iliyopita, Cheed na Killy waliwasilisha lalama zao kwa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kupata mwanga kuhusu sakata la kutimuliwa kwao. Lakini kikao cha kutatua mgogoro wao na lebo hiyo hakikuweza kufanyika baada ya uongozi wa Konde Music Worldwide kushindwa kufika Basata.

Read More
 Killy na Cheed waishtaki lebo ya Konde Music Worldwide kwa kuvunja mkataba wao

Killy na Cheed waishtaki lebo ya Konde Music Worldwide kwa kuvunja mkataba wao

Mambo yanazidi kuwa mengi baada ya wanamuziki Killy na Cheed kuondoshwa katika lebo ya muziki ya Konde Music Worldwide ambapo wasanii hao wameripotiwa kufika Baraza la Sanaa Tanzania BASATA kwa madai ya kufuatilia na kukamilisha mchakato wa kuachana na lebo hiyo. Meneja wa wasanii hao Sats Sembe, amesema sababu ya wao kufikisha malalamiko yao Basata ni kupinga utaratibu wa kuvunja mkataba na wasanii hao ambapo ameeleza kuwa hakuna barua yoyote ya maandishi waliopewa mpaka sasa. Sembe amesema kwa kuwa waliingia lebo ya Konde kwa maandishi basi hata kuondoka wanapaswa kuondoka kwa maandishi, ili kesho isije kutokea sintofahamu katika masuala ya kisheria. “Huko mbeleni hatujui hili suala litafika hapa, lakini kwa kuanzia tumeanzia kwa walezi wetu na wazazi wetu Basata ambao katika hali ya kawaida tusingeweza kuwaruka. “Lakini kama ikishindikana hatua hii tutaeda hata mahakamani ambapo kote huku barua ya maandishi ni muhimu kama ushahidi kwamba wameachana na wasanii”

Read More
 Cheed na Killy waondoka rasmi Konde Gang

Cheed na Killy waondoka rasmi Konde Gang

Lebo ya Konde Music Worldwide inayomilikiwa na Harmonize imetangaza rasmi kusitisha mkataba na wasanii wake wawili Cheed na Killy kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao. Lebo hiyo ambayo leo imetimiza miaka 4 tangu kuanzishwa kwake Oktoba 10, mwaka 2019, iliwasajili Cheed na Killy Septemba mwakaa 2020 wakitokea lebo ya King’s Music ya Ali Kiba Wasanii hao wanaungana na rapa Country Boy ambaye alijitoa Konde Music mapema mwa mwaka huu. Kwa miaka miwili waliyokuwepo Konde Music,Killy aliweza kutoa Greenlight EP yenye jumla ya nyimbo 5 huku Cheed akiachia Endless love EP yenye jumla ya ngoma 6 za moto.

Read More
 MSANII WA BONGOFLEVA KILLY AACHIA RASMI EXTENDED PLAYLIST (EP) YAKE MPYA

MSANII WA BONGOFLEVA KILLY AACHIA RASMI EXTENDED PLAYLIST (EP) YAKE MPYA

Mwanamuziki kutoka Konde Gang Worldwide Killy ameachia EP yake mpya inayokwenda kwa jina la The Green Light. Killy ameamua kuwa surprise mashabiki zake kwa kuachia EP hiyo mpya yenye nyimbo5 za moto huku ikiwa na kolabo mbili tu kutoka kwa Christian Bella, Harmonize na Ibraah. The Green Light EP ina nyimbo kama Ni Wewe, Vumilia, Kiuno, Itafika, Ilete, Niambie na itapatikana kwenye  Digital Platforms za kusambaza muziki duniani. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Killy amewashkuru maprodyuza na wasanii wenzake kwa kushirikiana nae kwenye mchakato wa kuiandaa ep hiyo. Hii inakuwa EP ya kwanza kutoka kwa mtu mzima Killy tangu atambulishwe kama msanii wa lebo ya muziki ya Konde Gang Worldwide inayomilikiwa na Harmonize.    

Read More
 MWANAMUZIKI WA BONGOFLEVA KILLY KUACHIA THE GREEN LIGHT EP IJUMAA HII

MWANAMUZIKI WA BONGOFLEVA KILLY KUACHIA THE GREEN LIGHT EP IJUMAA HII

Mwanamuziki wa Bongofleva Killy ametangaza tarehe mpya ya kuachia EP yake ya The Green Light. Kupitia ukurasa wake wa instagram Killy amesema Ep hiyo Itatoka rasmi Februari 25 siku ya Ijumaa ikiwa na jumla ya nyimbo 6 za moto. Msanii huyo wa Konde Gang amewaomba radhi mashabiki kwa kuisogeza mbele tarehe ya kutoka kwa EP hiyo ambayo ilipaswa kuachia Februari 20 mwaka huu kwa kusema kwamba kuna vitu havikuenda sawa kwa upande wake hivyo alilazimika kuahirisha shughuli ya kuachia The Green Light EP. Katika EP hiyo Killy amemshirikisha christian bella katika wimbo namba 6 uitwao ‘Niambie’, Ibraah katika wimbo namba 3 uitwao ‘Kiuno’ na boss wake harmonize katika lead singo yake iitwayo “Ni wewe” ambayo tayari imekwisha toka.

Read More
 KILLY AWAOMBA MASHABIKI WA KENYA WAMSAIDIE KUPATA ALIYEONDOA VIDEO YA WIMBO WAKE YOUTUBE

KILLY AWAOMBA MASHABIKI WA KENYA WAMSAIDIE KUPATA ALIYEONDOA VIDEO YA WIMBO WAKE YOUTUBE

Msanii wa Bongofleva, Killy amewaomba mashabiki wake waliyopo nchini Kenya kumsaidia kumpata Mutisya Munyithya ambaye ndiye ameipiga copy right YouTube video ya wimbo wake, Ni Yeye ambao amemshirikisha Harmonize. Mwimbaji huyo wa Konde Music Worldwide amewaomba mashabiki wanaomfahamu wawasiliane naye kwa namba +255 65 289 2317. “Mashabiki zangu pendwa poleni sana kwa maumivu ya kuondolewa kwa video yetu pendwa ya Ni Wewe. Hii ni moja ya changamoto tu katika kazi zetu japo inaumiza sana ila hatuna budi kuwa na subira”. “Ni changamoto ambayo ipo nje wa uwezo wangu ila Menejimenti ina shughulikia hilo na video yetu Ni Wewe itarudi tu soon, love you all my fans” amesema Killy. Hadi inaondolewa YouTube video hiyo ilikuwa na views zaidi ya milioni 2.

Read More
 VIDEO YA WIMBO WA KILLY “NI WEWE” YAFUTWA YOUTUBE KWA MADAI YA HAKIMILIKI

VIDEO YA WIMBO WA KILLY “NI WEWE” YAFUTWA YOUTUBE KWA MADAI YA HAKIMILIKI

Video ya wimbo wa Killy ‘Ni Wewe’ ambao amemshirikisha Harmoninze imeondolewa kwenye mtandao wa YouTube kutokana na malalamiko ya hakimiliki. Kwa sasa video hiyo haipatikani kwenye mtandao huo kufuatia malalamiko ya hakimiliki kutoka kwa Mutisya Munyithya. “This video is no longer available due to a copyrighty claims by Ian Mutisya Munyithya” taarifa ya YouTube inaeleza. Mdundo wa wimbo wa ni wewe wake killy  inafanana kwa kiasi kikubwa na wa wimbo maarufu wa zamani kundi la muziki la Les Wanyika, Sina makosa. Ikumbukwe mtandao wa Youtube hauruhusu kutumia kazi au kionjo cha mtu mwengine bila makubaliano.

Read More
 KILLY WA KONDE GANG WORLDWIDE ADOKEZA UJIO WA EXTENDED PLAYLIST YAKE

KILLY WA KONDE GANG WORLDWIDE ADOKEZA UJIO WA EXTENDED PLAYLIST YAKE

Nyota wa muziki wa bongofleva Killy ametangaza kuja na Extended Playlist ‘EP’ yake ,aliyoipa jina la ‘The Green Light ‘ inayotarajiwa kutoka ndani ya mwaka huu. Kupitia ukurasa wa instagram Hitmaker huyo wa ngoma ya ‘Ni Wewe’  amesema ‘EP’ hiyo ina jumla ya nyimbo 5 ,huku akiwa amewashirikisha wasanii wawili ambao ni  ibraah kutoka Konde Gang na Christian bella. Pamoja na kutangaza ujio wa EP hiyo Killy hajaweka wazi ni lini EP hiyo itatoka rasmi. Mpaka sasa mwanamuziki huyo anashikilia nafasi ya kwanza katika trending tab za mtandao wa YouTube nchini tanzania kupitia wimbo wake wa Ni wewe’ ambayo ina jumla ya views million 1.8.    

Read More