Baba wa Kimani Mbugua Akiri Mwanawe Alijitoa Uhai 

Baba wa Kimani Mbugua Akiri Mwanawe Alijitoa Uhai 

Baba mzazi wa mtangazaji wa zamani wa Citizen TV, Kimani Mbugua, amethibitisha kuwa mwanawe alijitoa uhai akiwa katika kituo cha rehab mjini Mombasa. Akizungumza na waandishi wa habari, baba huyo amesema kuwa hana lawama kwa mtu yeyote kufuatia kifo cha mwanawe, akieleza kuwa familia imepokea msiba huo kwa huzuni kubwa lakini kwa moyo wa kuvumilia. Aidha, ametoa onyo kwa Wakenya, akiwataka wasichukue hatua za kujitoa uhai kama suluhisho la changamoto wanazokabiliana nazo, bali watafute msaada na kuzungumza na watu wanaoweza kuwasaidia. Kimani Mbugua alikuwa akisumbuliwa kwa muda mrefu na matatizo ya afya ya akili, hali iliyosababisha apelekwe mara kadhaa katika vituo vya rehab katika juhudi za kumsaidia kurejea kwenye hali yake ya kawaida. Hata hivyo, juhudi hizo hazikuzaa matunda, na hatimaye alipoteza maisha akiwa katika kituo cha tiba huko Mombasa.

Read More