Noti Flow afunguka kuhusu afya ya mpenzi wake King Alami

Noti Flow afunguka kuhusu afya ya mpenzi wake King Alami

Rapa Noti Flow ameweka wazi namna mpenzi wake King Alami anaendelea hospitali mara baada ya kupata majeraha mabaya alipojirusha kutoka kwa jumba la ghorofa 7. Kupitia instastory yake amesema mrembo huyo anaendelea kupata nafuu na huenda madaktari wakamruhusu kurudi nyumbani hivi karibuni. Lakini pia amewataka mashabiki kumpa nafasi King Alami pindi atakaporejea kwenye mitandao ya kijamiii. Ikumbukwe kisa cha Kinga Alami kujirusha kutoka kwa jumba la ghorofa saba kisa kukataliwa na Noti Flow lilimpelekea kupoteza mkono wake wa kulia huku goti lake la mguu wa kulia likivunjika.

Read More
 Noti Flow ajutia kuvunja uhusiano wake na King Alami

Noti Flow ajutia kuvunja uhusiano wake na King Alami

Mwanamuziki mwenye utata nchini Noti Flow amekiri kuumia na kujutia kitendo cha kuvunja mahusiano yake na aliyekuwa mpenzi wake, King Alami. Kupitia ukurasa wake wa instagram Noti flow amesema mahusiano yao hayangevunjika huenda tukio la king alami kutaka kujiua kwa  kujirusha kutoka kwa jumba la ghorofa tano alingefanyika. Aidha amefichua kuwa watu wengi mitandaoni wanamlaumu kuwa yeye ndio chanzo cha kisa hicho kutokea huku akisema kuwa jumbe hizo zimemfanya ajihisi vibaya zaidi kwa hatua ya kumkimbia mrembo huyo ambaye walikuwa wanashiriki pamoja mapenzi ya jinsia moja. “We gon pray for you my baby We’ve been praying for you day & night . You’re strong my G & you’re still the coolest stud I fell in love with I love you more everyday Nothing’s changed & I’m with you thru it all.. I’m here for you forever my love. Quick recovery my baby you are loved and cherished ( for those who are blaming me thank you very much for making me feel worse & guilty than I already I’m. Y’all are right tho, it’s my fault cz if I was with her she’d be OK & safe like she’s always been so crucify me”. Ameandika Kauli yake imekuja siku moja baada ya kuwaomba wafuasi wake wamsaidie kuchangisha pesa za kugharamia matibabu ya aliyekuwa mpenzi wake, King Alami ambaye kwa sasa bado amelazwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta.

Read More
 Noti Flow aomba mchango wa kugharamia matibabu ya ex wake King Alami

Noti Flow aomba mchango wa kugharamia matibabu ya ex wake King Alami

Rapa Noti Flow ametoa wito kwa mashabiki na wahisani kuchangisha fedha za kugharamia matibabu ya mpenzi wake wa zamani King Alami. Kupitia ukurasa wake wa Instagram amechapisha bango ambalo limetoa taarifa zote ya jinsi mashabiki wanaweza fanikisha mchakato mzima wa kutoa mchango wao kwa mrembo huyo ambaye anadaiwa alijirusha kutoka kwa jumba la ghorofa 5 mwishoni mwa juma lililipota. Kuhusu hali ya King Alami ambaye amelazwa katika hospitali moja jijini Nairobi, Noti flow amedai kuwa kwa sasa hana ufahamu wa nini hasa kilimtokea Alami ila amewaachia maafisa usalama kufanya uchunguzi. Hata hivyo amewataka wanablogu kukoma kueneza propanganda mitandaoni kuhusu King Alami na badala yake wameweke kwa maombi wakati huu mgumu.

Read More
 Noti Flow awataka mashabiki kumuombea Ex wake King Alami baada ya kujirusha kutoka kwa jumba la ghorofa tano

Noti Flow awataka mashabiki kumuombea Ex wake King Alami baada ya kujirusha kutoka kwa jumba la ghorofa tano

Rapa Noti Flow ametoa wito kwa mashabiki zake kumuweka kwa maombi mpenzi wake wa zamani King Alami baada ya kudaiwa kuwa alijiangusha kutoka kwa jumba la ghorofa tano katika barabara ya Lumumba drive jijini nairobi. Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Noti Flow ambaye hajathibitisha madai hayo, amewataka walimwengu kuacha kueneza taarifa za uongo mtandaoni na badala yake wamuombee Alami na familia yake kwani kwa sasa wanapitia kipindi kigumu. Taarifa za King Alami kujiangusha kutoka kwa ghorofa zilitoka jana mara baada ya mtumiaji mmoja wa mitandao wa kijamii kuifahamisha mtandao wa udaku wa Nairobi Gossip kuwa mrembo huyo amekimbizwa katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta ambako anauguza majeraha mabaya. ” I understand there’s a lot of rumors going around the blog about my X gal. Kindly stop spreading unconfirmed info. The family is kindly requesting for privacy and prayers as we go through this tough time. My heart isbroken & I’m devastated but I’m staying positive and prayerful. Kindly do the same She needs it. I still hope its a dream,” Aliandika Instagram. Hata hivyo hajajulikana ni kitu gani hasa kilimpelekea King Alami kujirusha kutoka kwa jumba la ghorofa tano ila ni jambo la kusubiriwa. Utakumbuka juzi kati King Alami alijitokeza kwenye mitandao ya kijamii na kumuomba msamaha Noti Flow waweze kurudiana kwani amelikosa penzi lake baada ya mahusiano yao kuvunjika miezi 6 iliyopita kwa madai ya usaliti.

Read More
 Kng Alami akiri kutamani penzi la mpenzi wake wa zamani Noti Flow

Kng Alami akiri kutamani penzi la mpenzi wake wa zamani Noti Flow

Mrembo King Alami amekiri kulitamani penzi la mpenzi wake wa zamani msanii Noti Flow ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu jini mkata kamba alipoingilia mahusiano yao na kuwatenganisha. Kupitia video aliyochapisha kwenye ukarasa wake wa Instagram amesikika akijutia kuliacha penzi la Noti Flow kwa kusema kwamba tangu mahusiano yao yalipovunjika hajawahi pata furaha maishani kutokana na majuto ya vitendo vya usaliti alivyokuwa akishiriki kwa siri. Hata hivyo amemuomba radhi Noti Flow pamoja na mashabiki zake kwa hatua ya kwenda kinyume na kiapo cha mahusiano yao huku akimsihi ampe nafasi nyingine ya kumpenda kwani hatokuja kumuacha asilani. Utakumbuka King Alami na Noti Flow ambao wamekuwa gumzo nchini kwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja, walikuwa kwenye mahusiano kwa muda wa miezi 6 kabla ya penzi lao kuingiwa na ukungu kwa madai ya usaliti. Kipindi wawili hao wapo pamoja kama wapenzi walionyeshana upendo kiasi cha kila mmoja kuchora michoro ya tatoo kwenye miili yao lakini pia kuzawadiana vitu vya thamani ikiwemo gari kama njia ya kulifanya penzi lao libaki imara.

Read More