Msanii mpya toka King’s Music, Vanillah Music aachia rasmi EP yake mpya

Msanii mpya toka King’s Music, Vanillah Music aachia rasmi EP yake mpya

Mwimbaji mpya ndani ya lebo ya King’s Music Vanillah music aliyetambulishwa rasmi Novemba 3 mwaka huu na lebo hiyo, ameianza safari yake ya muziki akiwa na King’s Music kwa kuachia EP iitwayo “Listen To Me” yenye jumla ya ngoma 6. “Listen To Me” EP ina nyimbo kama Unanisitiri, Utachuma, Chizi, Nilimpemda Sana, Ananipigiania, Ayee na inapatikana kupitia digital plaforms zote za kuisikiliza mitandaoni. Kings Music kwa mwaka sasa imekuwa chini ya wasanii wanne; AliKiba, K2GA, Abdu Kiba na Tommy Flavour, hii ni baada ya kuondokewa na wasanii wawili, Killy na Cheed.

Read More
 Kings Music yatoa ratiba ya msanii wake Abdukiba.

Kings Music yatoa ratiba ya msanii wake Abdukiba.

Uongozi wa lebo yake ambao ni King’s Music imewekwa wazi ratiba ya msanii wake Abdu Kiba kuelekea mwishoni mwa mwaka 2022. Kwa mujibu wa ratiba hiyo ambayo Kings Music walichapisha kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram kabla mwaka haujaisha Abdu Kiba ataachia EP yake mpya. EP hiyo imetajwa kwenye ratiba itatoka Desemba 16, huku mwezi Novemba Abdu Kiba ataachia remix ya wimbo wake “Hainogi”. Lakini pia atakuwa na club tour mwishoni mwa mwaka ambapo atazunguka kwenye maeneo mbali mbali ya kukulia bat nchini Tanzania.

Read More