Kizz Daniel kuipiga “Buga” kwenye fainali za kombe la Dunia Qatar 2022

Kizz Daniel kuipiga “Buga” kwenye fainali za kombe la Dunia Qatar 2022

Mwanamuziki Kizz Daniel ametangaza kuwa atatumbuiza wimbo wake maarufu “BUGA” kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar. Hii ilikuwa ni ndoto ya Kizz Daniel tangu mwezi Juni mwaka huu ambapo kupitia Twitter, alianika wazi maombi yake akimuomba Mungu amsaidie kutimiza ndoto hiyo. Lakini pia Mwanamuziki huyo wa Nigeria ametangaza rasmi Jina la Album yake mpya, ameipa Jina la (Alcohol and Cigarettes) ambayo pia itafuatiwa na Ziara ya Muziki mwaka 2023 ambayo itakwenda kwa Jina hilo hilo.

Read More
 DAVIDO NA KIZZ DANIEL MBIONI KUACHIA EP YA PAMOJA

DAVIDO NA KIZZ DANIEL MBIONI KUACHIA EP YA PAMOJA

Mastaa kutoka Nigeria Davido na Kizz Daniel wamewadokezea mashabiki wa muziki wao juu ya ujio wa EP ya pamoja. Kupitia twitter wamethibitisha taarifa hiyo huku Davido akitamba kwamba EP hiyo itauza nakala milioni kwenye wiki ya kwanza. “Nani yuko tayari kwa ajili ya Ep ya 0.B.O X KIZZ?? Tutauza zaidi ya Milioni 1 katika wiki ya kwanza tu” ametweet Davido. Hata hivyo wawili hao hawajaweka wazi tarehe rasmi ya kuachia EP hiyo wala jina lake. Mara ya mwisho Wakali hao kukutana ilikuwa kwenye singo iitwayo “One Ticket” kutoka kwenye Album ya Kizz Daniel “No Bad Songz” ya mwaka 2018.

Read More