KLONS MELODY AFUNGUKA KUTOFAIDI NA MAPATO NYIMBO ZAKE SALDIDO

KLONS MELODY AFUNGUKA KUTOFAIDI NA MAPATO NYIMBO ZAKE SALDIDO

Aliyekuwa msanii wa Saldido International Klones Melody amefunguka tusiyoyajua kuhusu muziki wake akiwa chini ya lebo hiyo. Katika mahijiano na Presenter Ali, Klones amesema hajawahi pata mapato ya nyimbo zake zote alizofanya akiwa chini lebo ya saldido international i ayomilikiwa na Willy Paul. Amesema licha ya kumueleza Willy Paul kuhusu suala la miraba ya nyimbo zake bosi huyo hakuwahi taka kuweka wazi namna atakavyofaidi na mapato ya nyimbo alizofanya akiwa chini lebo hiyo kwani alianza kumchezea mchezo wa paka na panya. Hata hivyo ameenda mbali zaidi na kudai kuwa Willy Paul alimuondoa studio kwake kwa njia ya mabavu akiwa kwenye harakati za kuiandaa EP yake mpya jambo ambalo lilimkasirisha kiasa cha kufanya kuigura lebo hiyo. Hata hivyo amesema licha kwamba aliondoka kwenye lebo hiyo bila idhini yao mawakili wake wapo mbioni kuhakikisha anavunja kabisa mkataba wake wa miaka 5 na Saldido ila awe msanii wa kujitegemea. Utakumbuka Klones Melody alijiunga na saldido mwaka wa 2017 ambapo alisaini mkataba wa miaka mitano na lebo hiyo lakini alijiondoa miezi minne iliyopita baada ya kutofautia kimawazo na uongozi wa Saldido.

Read More
 KLONS MELODY AFUNGUKA MANYANYASO ALIYOYAPITIA CHINI SALDIDO INTERNATIONAL

KLONS MELODY AFUNGUKA MANYANYASO ALIYOYAPITIA CHINI SALDIDO INTERNATIONAL

Aliyekuwa msanii wa Willy Paul, Klons Melody amefunguka sababu zilizompelekea kujiondoa kwenye lebo ya muziki ya saldido international mwishoni mwa mwaka wa 2021. Katika mahojiano na Nicholas Kioko msanii huyo Willy Paul alikwenda kinyume na mkataba waliotia saini naye kipindi anajiunga na lebo hiyo, hivyo ikawa kizingiti kwake kufanikisha ndoto zake za kuupeleka muziki wake kwenye kiwango kingine. Klons Melody ambaye anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao BIMA amedai kwamba alipokuwa chini ya saldido Willy Paul alibana sana asijihusishe na masuala ya muziki kwani mara nyingi alijipata anafanya usafi na kupika chai jambo ambalo anadai lilimpa msukumo wa kuondoka Saldido. Hata hivyo amesema licha ya kwamba alipitia manyanyaso kwa mikono ya Willy Paul ataendelea kumpa heshima kwa kuwa alimshika mkono na kumtambulisha kwenye tasnia ya muziki hadi mashabiki wakamfahamu. Utakumbuka Klons Melody alijiunga na lebo ya Saldido inayomilikiwa na Willy Paul mwaka wa 2017, na chini lebo hiyo alifanikiwa kushirikishwa kwenye nyimbo mbili ambazo ni Odi Love, na Atoti Jaber.

Read More