KOLABO YA NYASHINSKI NA FEMI ONE KUACHIWA RASMI IJUMAA HII
Staa wa muziki nchini Nyashinski ametangaza ujio wa ngoma yake mpya ambayo amemshirikisha mkali wa muziki nchini Femi one. Kupitia ukurasa wake wa instagram Nyashinski ameandika ujumbe unaosomeka PROPERLY!!!! This FRIDAY 26.11.2021. You Ready? akiashiria kwamba mashabiki wake wakae mkao wa kula kuupokea wimbo wake na femi uitwao properly ambao utatoka rasmi ijumaa hii Novemba 26 mwaka wa 2021 Hii itakuwa kazi ya kwanza kwa Nyashinski na Femi One ikizingatiwa kuwa wawili hao hawajai fanya wimbo wa pamoja. Ikumbukwe Nyashinski amekuwa ukimya kwa takriban miezi 7 tangu aachie ep yake iitwayo Hatrick iliyokuwa na mikwaju 3 ya moto.
Read More