Lady Jaydee kuzindua album yake mpya mwezi Februari

Lady Jaydee kuzindua album yake mpya mwezi Februari

Msanii mkongwe wa Bongofleva, Lady Jaydee ametangaza ujio wa album yake mpya iitwayo “Love Sentence” ambayo amemshirikisha msanii mwenzake Rama Dee. Jide amesema, album yao ina jumla ya nyimbo 10 zote zikiwa za mapenzi ambapo amefichua kuwa nyimbo 2 ambazo ni Matozo na I Found Love tayari zimeshatoka. Uzinduzi wa album hiyo utafanyika Februari 10, mwaka 2023 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

Read More
 Lady Jaydee mbioni kuja na documentary ya maisha yake

Lady Jaydee mbioni kuja na documentary ya maisha yake

Msanii mkongwe wa Bongofleva Lady Jaydee ametangaza ujio wa documentary yake ambayo ana mpango wa kuachia hivi karibuni. Lady Jaydee ameshare habari hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kusema kwamba documentary itatujuza mengi zaidi kuhusu safari ya maisha yake hadi kuwa maarufu na mchango wake kwenye game ya bongofleva. “Wote mnaoongea hayo hamnifahamu hata kidogo na nikianza kumuelezea mmoja mmoja nitaota mvi zaidi ya hizi nilizonazo” “Nawasihi mvumilie hadi nitakapotoa documentary ya maisha yangu ili wote mpate kufahamu mnachohitaji toka kwangu.” Ameandika Lady Jaydee akimjibu shabiki.

Read More
 Lady Jaydee adokeza ujio wa Album ya pamoja na Rama Dee

Lady Jaydee adokeza ujio wa Album ya pamoja na Rama Dee

Mkongwe wa muziki wa Bongofleva, Lady Jaydee ametangaza ujio wa album ya pamoja na msanii mwenzake Rama Dee. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Jide ambaye ni mwimbaji wa kike wa Bongofleva anayeongoza kutoa album nyingi zaidi akiwa nazo nane, amesema album hiyo itaingia sokoni mwezi huu kabla ya tamasha lake la muziki. Lady Jaydee kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao “Suluhu” aliomshirikisha Rama Dee, ikiwa ni wimbo wao wa pili kuachia baada ya”Kama Hauwezi” iliyotoka mwaka 2017.

Read More