Lava Lava Alalamika Kufanyiwa Fitina na Wasanii Wenzake
Msanii wa Bongo Fleva Lava Lava amefunguka kwa hisia kupitia ukurasa wake wa Instagram akidai kuwa yeye ndiye msanii pekee anayeongoza kwa kufanyiwa fitina kila mara anapotoa kazi mpya. Kupitia ujumbe wake wa moja kwa moja, Lava Lava alisema mara nyingi nyimbo zake hukumbana na vikwazo vinavyowekwa na wasanii wenzake, lakini akasisitiza kwamba hali hiyo haijamkatisha tamaa kwani anaamini Mungu yupo upande wake na ataendelea kumpigania. Kauli yake imechochea mjadala mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakimuunga mkono wakisema changamoto ni sehemu ya safari ya mafanikio, huku wengine wakimkosoa wakidai analalamika badala ya kuendelea kuweka nguvu katika kazi zake. Lava Lava, anayejulikana kwa sauti yake laini na nyimbo zinazopenya haraka kwenye soko, ameendelea kudhihirisha kwamba licha ya changamoto za fitina, bado ana imani kubwa na safari yake ya muziki.
Read More