Leila Kayondo na mpenzi wake wa zamani SK mbuga wafufua tena penzi lao

Leila Kayondo na mpenzi wake wa zamani SK mbuga wafufua tena penzi lao

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Leila Kayondo amethibitisha kumaliza tofauti zake na mpenzi wake wa zamani SK mbuga baada ya wawili hao kutupiana maneno makali mtandaoni. Kupitia mahojiano yake Kayondo amesema kwa sasa yeye na SK Mbuga ni marafiki wakubwa huku akidai kuwa huwa wanazungumza mara kwa mara kuhusu masuala ya kibiashara na maisha kwa ujumla. Mrembo huyo amesisitiza kuwa hakuna mtu atakayevunja urafiki wao kamwe, kitendo ambacho walimwengu wamehoji kuwa huenda amefufua tena penzi lake kwa bwenyenye huyo mwenye skendo nyingi za kutoka kimapenzi na wanawake tofauti. Utakumbuka miezi kadhaa iliyopita Leila Kayondo alikuwa gumzo nchini Uganda baada ya video kusambaa mitandaoni ikimuonyesha akitema nyongo kwa SK Mbuga kuwa asiwahi kayaga nyumbani kwake ambapo alienda mbali zaidi na kutishia kuanika maovu aliyomfanyia kipindi wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi mwaka 2010 hadi 2015.

Read More
 LEILA KAYONDO AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA SK MBUGA

LEILA KAYONDO AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA SK MBUGA

Mwanamuziki kutoka uganda Leila Kayondo na bwenyenye SK Mbuga walikuwa wapenzi mwaka wa 2012 hadi 2015 walipovunja mahusiano baada ya kuingia kwenye ugomvi mkali. Leila alimtuhumu SK kwa kumnyanyasa kijinsia kwa kumshushia kipigo kila mara na akaamua kumuacha kabisa. Lakini cha kushangaza amejitokeza sasa na kudai kwamba hakuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na bwenyenye huyo ikizingatiwa kuwa walikuwa wanafurahia maisha pamoja. “Sijawahi chumbiana na Sk Mbuga. Tulikuwa tu tunafurahia maisha.”,Alisema kwenye mahojiano na  runinga ya NBS . Hata hivyo SK Mbuga hajatoa kauli yoyote kuhusu madai yaliyoibuliwa na msanii huyo ikizingatiwa kipindi cha nyuma jamaa huyo alimzawadi gari aina BMW kama njia ya kumuonyesha mapenzi.

Read More