Socialite Liebe Kiki Awaonya Wasichana Wanaotaka Kujichubua: “Hakikisha Una Pesa ya Kutosha”
Socialite maarufu Liebe Kiki ametoa ushauri kwa wasichana wanaotamani kujichubua ngozi, akisema kuwa mchakato huo ni wa gharama kubwa na unahitaji maandalizi ya kifedha ya kutosha. Kupitia video iliyosambaa mitandaoni, Liebe Kiki alisema kwamba kujichubua si jambo la mchezo na ni lazima mtu awe na uwezo wa kifedha wa kuendeleza matunzo ya ngozi kwa muda mrefu, la sivyo atajikuta katika hali mbaya zaidi kiafya na kimuonekano. “Kujichubua ni gharama. Kama huna pesa za kutosha, tafadhali usianze. Itakupeleka pabaya zaidi kuliko ulivyokuwa,” alisema Kiki. Socialite huyo aliongeza kuwa wasichana wengi huingia kwenye safari ya kujichubua bila kuelewa kikamilifu kile kinachohitajika, na matokeo yake huishia kuwa na matatizo ya ngozi kama vipele, kuchomwa na kemikali, au mabadiliko mabaya ya rangi ya ngozi. Hii si mara ya kwanza kwa Kiki kutoa maoni kuhusu mitindo ya urembo. Amekuwa mstari wa mbele kuzungumzia upasuaji wa kuongeza makalio, maisha ya mitandaoni, na changamoto wanazopitia wanawake maarufu.
Read More