“Kifo cha PNB Rock kimenifanya niwe muoga”- Asema Lil Baby

“Kifo cha PNB Rock kimenifanya niwe muoga”- Asema Lil Baby

Rapa Lil Baby amefunguka na kusema kuwa baada ya kupata habari za kifo cha rapa mwenzake Pnb Rock kilichotokea Septemba 12 mwaka huu, amekuwa muoga hata wa kutoka nje. Kupitia mahojiano aliyoyafanya na complex, Lil Baby amesema “Imekuwa kama simu ya kuniamsha, sio kwamba sijui kuna matukio kama hayo ila taarifa za kifo cha Pnb Rock zimenifanya niwe muoga hata wa kwenda kula kwenye migahawa mikubwa pia imenifanya niwe makini zaidi” Utakumbuka Rapa PNB Rock aliuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia Septemba 12 kwenye tukio la uvamizi lililotokea kwenye mgahawa mmoja Jijini Los Angeles.

Read More
 LIL BABY ASHINDA MILLIONI 120 ZA KENYA KUPITIA KAMARI

LIL BABY ASHINDA MILLIONI 120 ZA KENYA KUPITIA KAMARI

Staa wa muziki kutoka Marekani Lil Baby ameshinda takriban shillingi millioni 120 za Kenya kwenye mchezo wa bahati nasibu maarufu Casino. Baada ya kushinda mkwanja huo, Lil Baby amewabariki washkaji zake kwa kuwapa shillingi millioni 1.2 kila mmoja. Kupitia Twitter Lil Baby ameachia ujumbe usemao “Wanajua nimeshinda pesa, lakini wasichokijua ni kwamba sipo hapa kula bata, ninawekeza.” Kwa wasiofahamu, Lil Baby alikuwa mcheza kamari mzuri tu kabla ya kuingia kwenye muziki.

Read More
 LIL BABY NA CHRIS BROWN MBIONI KUJA NA TAMASHA LIITWALO ONE OF THEM ONES

LIL BABY NA CHRIS BROWN MBIONI KUJA NA TAMASHA LIITWALO ONE OF THEM ONES

Wasanii kutoka marekani Chris Brown na Lil Baby wametangaza kuja na ziara ya pamoja ambayo wameipa jina la “One Of Them Ones”. Ziara hiyo itapita kwenye miji 27 nchini Marekani na imepangwa kuanza Julai 15 na kumalizika Agosti 27 mwaka huu. Kwa upande wa Chris Brown, ziara hii inakuja huku kukiwa na tetesi za ujio wa Album yake mpya iitwayo “Breezy” ambapo tayari ameachia mkwaju mmoja uitao ‘WE (Warm Embrace)’ na hajafanya ziara tangu mwaka 2019 alipofanya Indigo Tour. Kwa Lil Baby vile vile naye anatarajiwa kuachia Album mpya kwani tayari amedondosha ngoma mbili; ambazo ni  “Right On” na “In a Minute.”

Read More