Serikali Yakanusha Utetezi wa Lil Durk Kuhusu Mistari ya Muziki

Serikali Yakanusha Utetezi wa Lil Durk Kuhusu Mistari ya Muziki

Mamlaka za Marekani zimejibu vikali utetezi wa rapa Lil Durk, ambaye anadai kuwa analengwa kwa sababu ya mistari ya nyimbo zake, si kwa makosa ya jinai. Katika taarifa yao, waendesha mashtaka wameweka wazi kuwa Durk hashtakiwi kwa sababu ya muziki wake, bali kwa madai ya kupanga njama ya mauaji ya kikatili, iliyotokea mwaka 2022 dhidi ya rapa mwenzake Quando Rondo, na kupelekea kifo cha mtu mmoja. Hii ni baada ya wakili wa Durk kudai kuwa msanii huyo anaonewa na kuwa serikali ina jaribu kuchukulia ubunifu kama uhalifu, kwa kutumia mistari ya nyimbo kama ushahidi wa jinai. Hata hivyo, waendesha mashtaka wamesema kuwa hata baada ya kuondoa mistari ya muziki kutoka kwenye hati mpya ya mashtaka, bado kuna ushahidi wa kutosha kumhusisha Durk na shambulio hilo. Kwa upande wake, timu ya mawakili wa Durk inaendelea kupambana mahakamani, ikiomba kesi ifutwe na pia kusisitiza apewe dhamana akisubiri kesi yake iliyopangwa kusikizwa Oktoba mwaka huu. Wakati mashabiki wakisubiri kuona mwelekeo wa kesi hii, gumzo linaendelea kuhusu uhuru wa wasanii kuzungumza kupitia muziki bila kuogopa kufunguliwa mashtaka.

Read More
 RAPPER LIL DURK AWATAHADHARISHA WANAOTAKA KUACHIA KAZI ZAO IJUMAA HII

RAPPER LIL DURK AWATAHADHARISHA WANAOTAKA KUACHIA KAZI ZAO IJUMAA HII

Rapa kutoka Marekani Lil Durk amewapa tahadhari wasanii wanzake ambao nao wanamipango ya kuachia kazi zao mpya ijumaa ya wiki hii. Kupitia ukurasa wake wa Instagram rapa huyo ambaye ni mzaliwa wa Chicago, Illinois ameweka wazi kuwa album yake ya “7220” haita ahirishwa tena na yeyote atakayetaka kuachia album yake Machi 11 mwaka huu ajipange kwa kuwa amejipanga kuuza zaidi ya wote watakaoachia album siku hiyo Hayo yanajiri ikiwa ni wiki kadhaa zimepita tangu asogeze mbele tarehe ya kuachia album yake mpya iitwayo “7220” ambayo ilikuwa itoke Februari 22, tarehe moja na album ya Kanye West, akakubali yaishe akasogeza mbele album yake.

Read More
 BIFU LA RAPA LIL DURK NA NBA YOUNGBOY LACHUKUA SURA MPYA

BIFU LA RAPA LIL DURK NA NBA YOUNGBOY LACHUKUA SURA MPYA

Rapa kutoka nchini Marekani Lil Durk amevunja kimya chake kuhusu kinachoendelea mtandaoni kati yake na NBA Youngboy. Lil Durk kupitia ukurasa wake wa instagram amepost picha akiwa amelalia pesa nyingi na kuandika ujumbe “mpuuzi” uliotafsiriwa kuwa ni jibu kwa NBA Youngboy Lil Durk ametoa kauli hiyo baada ya rapa NBA Youngboy kum-diss pamoja na label ya O’block kwenye ngoma yake mpya Bring The Hook & Know Like I Know ambapo amewatolea kauli chafu lakini pia kumtishia lil durk kwamba atakufa “young n**ga gone die…stay safe” Lakini pia kupitia ngoma hiyo amem-diss rapa nlechoppa kwa kuingilia bifu kati yake na watu wa (o’block) label inayomilikiwa na lildurk, akidai kwamba anaingilia bifu lisilomhusu NBA Youngboy kupitia ngoma hiyo amesikika kwenye mstari akisema (you could say i was you favourite n**ga better stay up in your place b****h) yaani ulisema kwamba ulikuwa unanikubali lakini ni bora ukabaki katika nafasi yako mpuuzi wewe. Utakumbuka NBA Young aliachia disstrack hiyo kufuatia NLE Choppa kumtwanga ngumi shabiki yake baada ya kuingia kwenye ugomvi  wakiwa uwanja wa ndege. Sababu ya ugomvi huo inasemekana kuwa ni baada ya NLE Choppa kufanya moja ya interview hivi karibuni na kusema kwamba hapo awali NBA Young boy alikuwa moja kati ya wasanii wake anaowakubali zaidi lakini kutokana na ngoma yake mpya “Bring the Hook” aliyowa-diss  genge la O’block na marehemu King Von ameamua kumkataa

Read More
 LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 14, ALIZALIWA RAPA KUTOKA MAREKANI LIL DURK

LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 14, ALIZALIWA RAPA KUTOKA MAREKANI LIL DURK

Siku kama ya leo Oktoba 19 mwaka wa 1996 alizaliwa  staa wa muziki wa Hiphop na mwaandishi wa nyimbo kutoka nchini Marekani Lil Durk. Jina lake halisi ni Durk Derrick na alizaliwa huko Chicago Illinois nchini Marekani ambako alianza muziki mwaka wa 2009 lakini alikuja akapataa umaarufu mwaka wa 2011 baada ya kuachia ngoma zake mbili ambazo ni Sneak Dissin na Ima  Hitta zilizopokelewa kwa ukubwa nchini Marekani. Mwaka wa 2012 Lil Durk aliachia mixtape yake inayokwenda kwa jina la   Life Aaint No Joke chini ya lebo ya muziki ya OTF  ikafuatwa na mixtape yake iitwayo Signed To The Street ya mwaka wa 2013 ambayo ilitayarishwa na lebo ya muziki ya Def  Jam  Recordings. Mwaka wa 2014 Lil Durk aliachia mixtape nyingine iitwayo The Sequel to Signed to the Streets ikafuatwa na album yake ya kwanza ya mwaka wa 2015 iitwayo Remember My Name, album ambayo ilikuwa na jumla ya ngoma 10 za moto. Mwaka huo huo wa 2015 Lil Durk aliachia mixtape yake inayokwenda kwa jina la 300 days, 300 Nights ambayo ilikuwa ngoma kama My Beyonce ambayo iliweza kufikia viwango vya mauzo ya gold kwa kuuza zaidi ya nakala laki 5. Mwaka wa 2016 Lil Durk aliachia album yake ya pili iitwayo Lil Durk  2X ambayo ilikuwa na jumla ya ngoma 11 akiwa  amewashirikisha wasaani kama young thug,ty dolla sign na wengine kibao. Hata hivyo tangu Lil Durk aanze kujishughulisha na muziki wa hiphop nchini Marekani mwaka wa 2009 amefanikiwa kufanya jumla ya album tano za muziki,Mixtape 12,Singles 20 na album mbili iliyobeba nyimbo zilitoka pamoja na zile hazikutoka. Lil Durk kwa sasa amesainiwa na lebo ya muziki ya Def Jam Records lakini pia yupo chini ya record lebo  ya Coke Boys inayomilikiwa na rapa French Montana ambayo inafanya kazi pamoja na lebo yake ya muziki ya Only the Family.

Read More