LIL DUVAL APINGA BLAC CHYNA KUINGIZA KSHS. BILLIONI 2.4 KUPITIA ONLYFANS

LIL DUVAL APINGA BLAC CHYNA KUINGIZA KSHS. BILLIONI 2.4 KUPITIA ONLYFANS

Mchekeshaji na Muigizaji Lil Duval ameibuka na kuzungumzia ishu ya Blac Chyna kutengeneza zaidi ya KSh. Bilioni 2.4 kila mwezi mwaka 2021 kwenye mtandao wa OnlyFans. Kupitia mfululizo wa post zake kwenye mitandao ya kijamii, Mchekeshaji huyo amesema huu ni uzushi mtupu na hakuna ukweli wowote. “Siamini kama nyie wote mnaamini Blac Chyna alitengeneza kiasi hicho cha pesa ($20 million) kwa mwezi kupitia OnlyFans. Hapa ndio nafahamu sasa ninyi nyote hamuishi kwenye uhalisia.” aliandika Lil Duval na kucheka kisha kuongeza “Mnaamini kila mnachokiona kwenye vichwa vya habari, na hata hamuulizi. Nimeona Wanawake waki-post na kusema ‘Naweza kuamini’ hii ni ushahidi kwamba nyie wote hamjui ($20 Million) ilivyo. Mmiliki wa OnlyFans ameanika hilo ili kuwapumbaza vichwa vyenu na mfungue akaunti zenu. Namba hazidanganyi, lakini kwa hili wametupanga.” alimalizia Lil Duval.

Read More
 LIL DUVAL AKERWA NA KITENDO CHA WANAWAKE MAREKANI KUWABAMBIKIA KESI ZA UBAKAJI BAADHI YA WANAUME

LIL DUVAL AKERWA NA KITENDO CHA WANAWAKE MAREKANI KUWABAMBIKIA KESI ZA UBAKAJI BAADHI YA WANAUME

Mchekeshaji Lil Duval kutoka nchini Marekani, ameonesha kukerwa na kitendo cha baadhi ya wanawake kuwabambikia kesi za ubakaji baadhi ya wanaume maarufu nchini humo. Duval amesema hayo huku akitolea mfano sakata la sasa lililomkuta Chris Brown, akishutumiwa kumbaka mwanamke mmoja ambaye hakutajwa jina huku baadhi ya taarifa na ushahidi zikimuonesha mwanamke huyo, akimuomba Chris kufanya nae tendo la ndoa kwa hiyari. Mchekeshaji huyo amesisitiza kuwa anatamani kuona siku moja wanawake wakiwajibishwa kwa kutoa tuhuma za uongo dhidi ya wanaume, ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vinazidi kuongezeka kwa kasi nchini Marekani.

Read More