Mtoto wa Lil Wayne Asema Baba Yake Ndiyo Msingi wa Mafanikio ya Drake

Mtoto wa Lil Wayne Asema Baba Yake Ndiyo Msingi wa Mafanikio ya Drake

Mtoto wa rapa maarufu Lil Wayne, anayefahamika kwa jina la kisanii Lil Novi, amezua gumzo mitandaoni baada ya kudai kuwa mafanikio ya rapa Drake yalichangiwa pakubwa na mchango wa baba yake katika uandishi wa nyimbo. Akizungumza katika mahojiano maalum yaliyopeperushwa hivi majuzi, Lil Novi alisema kuwa Lil Wayne hakuhusika tu kumtambulisha Drake kwa dunia ya muziki, bali pia alihusika moja kwa moja katika kuandika nyimbo zake nyingi zilizomletea umaarufu mkubwa.  “Baba yangu ndiye aliyeweka msingi mzuri kwa Drake. Yeye ndiye aliyemsaidia kuandika nyimbo nyingi za Drake ambazo zimepata mafanikio makubwa,” alisema Lil Novi kwa msisitizo. Kauli hiyo imeibua mijadala mikali miongoni mwa mashabiki wa hip hop, huku baadhi wakisema kwamba si jambo la kushangaza ikizingatiwa kuwa Lil Wayne ndiye aliyemsaini Drake chini ya lebo yake ya Young Money mwaka 2009, kipindi ambacho Drake alikuwa bado hajajijengea jina kimataifa. Uhusiano kati ya Lil Wayne na Drake umeendelea kuvutia hisia za wengi, hasa kutokana na ushirikiano wao wa muda mrefu na mafanikio ya pamoja katika muziki. Hata hivyo, madai ya Lil Novi yanaweza kufungua ukurasa mpya wa mjadala kuhusu mchango wa Lil Wayne katika mafanikio ya Drake, ambao kwa sasa ni miongoni mwa wasanii wa hip hop wanaosikilizwa zaidi duniani. Wakati mashabiki wakingoja kauli ya Drake au Lil Wayne kuhusu suala hilo, ukweli mmoja unabaki palepale, ushawishi wa Lil Wayne katika muziki wa kizazi hiki hauwezi kupuuzwa.

Read More
 Lil Wayne ashtakiwa na mpishi wake

Lil Wayne ashtakiwa na mpishi wake

Rapa Lil Wayne ameshtakiwa na mpishi wake wa zamani ambaye amedai kwamba alifukuzwa kazi kimakosa kwasababu alienda kumuuguza mwanae mwenye umri wa miaka 10.Kwa mujibu wa Blast mpishi huyo Morgan Medlock  anasema kwamba alifukuzwa kazi baada ya kuondoka pale alipogundua kuwa mtoto wake amepata majeraha ya kichwa Morgan ambaye kwa wakati huo alikuwa mjini Las Vegas pamoja na Wayne, ameeleza kwenye nyaraka zake za mahakama kwamba alitaka kurudi Los Angeles akakae na mtoto wake lakini ndege ilikuwa imechelewa kuondoka kwasababu wayne alikuwa busy sana akivuta ndani ya ndege na hivyo kuamua kuchukua ndege nyingine na kuambiwa atoe taarifa pale atakapokuwa na mwanae Alipoulizwa kama ataachana na kazi hiyo Morgan alisema hapana hana nia ya kuacha kazi kwa muda huo ambapo alijibu kwa njia ya meseji “No” baada ya muda mfupi alishangaa amejibiwa “goodbye” “Tell Morgan this isn’t going to work” . Jibu la Lil Wayne kwa msaidizi wake akitaka amwambie mpishi huyo kuwa hawataendelea nae kikazi Morghan alishangazwa kabisa na kuvunjwa kwa mkataba wake ghafla, na hivyo aliamua kufungua kesi akidai fidia zaidi ya Ksh.Milioni 56.8

Read More
 Lollipop ya Lil Wayne yafikia mauzo ya Diamond

Lollipop ya Lil Wayne yafikia mauzo ya Diamond

Rapa kutoka Marekani Lil Wayne amefikia rekodi ya mauzo ya Diamond ambayo ameinasa kupitia single yake “Lollipop” iliyotoka mwaka 2008. “Lollipop” ambayo Lil Wayne alimshirikisha Static Major ambaye alifariki wiki mbili kabla ya kuachiwa kwa wimbo huo, unakuwa wimbo wa kwanza kwa mtu mzima Wayne kufikia mauzo hayo. Sanjari na hilo, wimbo huo ndio wimbo wenye mafanikio zaidi katika maisha ya muziki ya Lil wayne ambapo ulitajwa kuifanya album yake ya “Tha Careter III” kuuza zaidi ya Units Million Moja katika wiki yake ya kwanza na kunyakua tuzo ya Grammy mwaka 2009 kama Best Rap Song.

Read More
 LIL WAYNE ATANGAZA TAREHE YA KUFANYIKA KWA LIL WEEZYANA FESTIVAL

LIL WAYNE ATANGAZA TAREHE YA KUFANYIKA KWA LIL WEEZYANA FESTIVAL

Rapa Lil Wayne ametangaza ujio wa awamu ya sita wa tamasha lake la “Lil WeezyAna Festival” huko New Orleans nchini Marekani. Tamasha hilo ambalo mwaka 2019 ndio ilikuwa mara yake ya mwisho kufanyika baada ya katazo la mikusanyiko kutokana na janga la Corona, sasa linarudi kivingine mwaka huu na litafanyika Agosti, 27 katika eneo la Champion’s Square. Kikubwa ambacho Lil Wayne anajivunia kutokana na tamasha hilo ni kwamba sehemu ya pesa ambazo zitakusanywa kutokana na mauzo ya tiketi zitatumika kufadhili elimu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya eneo hilo la New Orleans Louisiana ambalo ni nyumbani kwao. Rais wa kampuni ya muziki ya Lil Wayne iitwayo Young Money Records, Mack Maine ambaye pia ni rappa, kwenye mahojiano na COMPLEX amesema atatumia fursa ya tamasha hilo kutoa heshima kwa waliopoteza maisha kwenye kimbunga cha Katrina miaka 17 iliyopita. Lakini pia amesema kwenye msimu huu wa sita wa tamasha hilo kutahudhuriwa pia na wageni maalumu.

Read More
 LIL WAYNE APIGWA MARUFUKU KUTUMBUIZA UINGEREZA

LIL WAYNE APIGWA MARUFUKU KUTUMBUIZA UINGEREZA

Rapa Lil Wayne amezuiliwa kuingia nchini Uingereza kuelekea kwenye tamasha la Strawberries & Creem. Waandaaji wa tamasha hilo wametoa taarifa isemayo, Lil Wayne amezuiliwa dakika za mwisho na wamesikitishwa na uamuzi huo wa wizara ya Mambo ya Ndani kwani Wizzy alikuwa msanii Kinara wa tamasha hilo. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Uingereza ameiambia tovuti ya Rolling Stone kwamba, mtu yeyote ambaye aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miezi 12 au zaidi, maombi yake kuingia nchini humo yatatupiliwa mbali. Utakumbuka Mwaka 2007 Lil Wayne aliwahi kukamatwa kwa makosa ya silaha ambapo alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja Jela lakini aliachiwa baada ya miezi 8 kutokana na mwenendo mzuri.

Read More
 MLINZI WA LIL WAYNE AFUNGUA MASHTAKA BAADA YA KUTISHIWA SILAHA NA RAPA HUYO

MLINZI WA LIL WAYNE AFUNGUA MASHTAKA BAADA YA KUTISHIWA SILAHA NA RAPA HUYO

Mlinzi wa rapa Lil Wayne kutoka Marekani ameamua kutimba mahakamani na kufungua mashtaka dhidi ya Lil Wayne ambaye anadaiwa kumtishia silaha mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka wa 2021. Kwa mujibu wa TMZ, moja ya walinzi wa rapa huyo aliwaambia polisi kwamba  Lil Wayne aliingia kwenye majibizano na bodyguard wake akiwa nyumbani kwake mjini Hidden Hills, California. Hii ni baada ya Lil Wayne kumtuhumu bodyguard huyo kupiga picha ya nyumba yake na kuzivujisha kwenye vyombo vya habari.

Read More