JULIANI AKIRI KUPOTEZA DILI NONO KISA MKE WAKE LILIAN NG’ANG’A

JULIANI AKIRI KUPOTEZA DILI NONO KISA MKE WAKE LILIAN NG’ANG’A

Rapa kutoka Kenya Juliani amefichua kuwa alipoteza dili mbili kubwa baada ya kuingia kwenye mahusiano ya kimpenzi na Lilian Ng’ang’a mwaka 2021. Akizungumza na Kalondu Musyimi, Juliani amesema makampuni yalioyolenga kufanya nae kazi kipindi hicho yaliingiwa na hofu kutokana na namna watu walivyokuwa wakimshambulia mtandaoni. Juliani hata hivyo ametoa changamoto kwa vyombo vya habari kuwakuza wasanii wa Kenya badala ya kuwapigia simu pale wanapofuatilia habari za udaku. Mapema wiki hii Juliani aliingia kwenye vichwa vya habari za burudani baada ya baadhi ya watumiaji mitandao ya kijamii kumfananisha na aliyekuwa gavana wa Machakos Alfred Mutua ambaye awali alikuwa akichumbiana na Lilian Ng’ang’a. Walimwengu walienda mbali zaidi na kuhoji ni kwa nini Lilian aliamua kumwacha Mutua mwenye utajiri mkubwa na kuishia kuingia kwenye mahusiano na Juliani ambaye walidai anasuasua kiuchumi.

Read More
 JULIANI AWAJIBU KISOMI WANAOIPONDA MAHUSIANO YAKE NA LILIAN NGANGA

JULIANI AWAJIBU KISOMI WANAOIPONDA MAHUSIANO YAKE NA LILIAN NGANGA

Hatimaye mwanamuziki Juliani amefunguka kuhusu kinachoendelea mitandaoni kumuhusu mke wake Lilian Ng’ang’a. Kupitia ukurasa wake wa twitter ameamua kutoa maelezo kuhusu hali yake ya uchumi kwa kuwakejeli wanaomsema vibaya mtandaoni. Rapa huyo ameandika ujumbe anaosema kwamba amefulia kiuchumi ambapo ameenda mbali zaidi na kuwaomba wakenya msaada wa kifedha kupitia paybill ili aweze kumnunulia mtoto wake pampers. “Wase! Nikubaya niko BROKE! mtoi anahitaji pampers. Please send mpesa. Paybill: Business number – 784577 Account- Juliani Chochote unaeza itasaidia. Yours truly, Struggling rapper/entrepreneur”, Ameandika Juliani. Ujumbe huo umezua hisia mseto miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii wengi wakihoji kuwa huenda amewajibu kimtindo wanaodai kuwa anaishi maisha ya uchochole huku wengine wakimshushia kila aina matusi kwa hatua ya kukimbia na mke wa Alfred Mutua.

Read More
 LILIAN NG’ANG’A AWACHANA WANAOISEMA VIBAYA NDOA YAKE NA JULIANI

LILIAN NG’ANG’A AWACHANA WANAOISEMA VIBAYA NDOA YAKE NA JULIANI

Mke wa Juliani, Lilian Ng’ang’a ameshindwa kuwavumilia watu wanaozidi kumkejeli mtandaoni kwa hatua ya kuingia kwenye ndoa na mwimbaji huyo. Kilichomuumiza zaidi mrembo huyo ni kitendo cha watu kuhoji kuwa ilikuwa ni fedhea kwake kuacha utajiri wa Alfred Mutua na kisha kukimbilia maisha ya taabu kwa Juliani. Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Ng”ang’a ameonekana kukerwa na watu wanaomsema vibaya mtandaoni kwa kuandika ujumbe uliotafsiri kuwa hajutii kumuacha Mutua na kumpenda Juliani ambaye ni mwanamuziki. Lilian ambaye amejaliwa kupata mtoto na Juliani amesema hana muda kabisa wa kupishana na walimwengu ambao hawana shughuli ya kufanya mtandaoni huku akiwataka waendelea kumsema vibaya kwani hana uwezo wa kuthibiti kile wanachomuwazia. Kauli ya Lilian Ng’ang’a inakuja mara baada ya watu kulinganisha utajiri wa mpenzi wake wa sasa Juliani na mume wake wa zamani Alfred Mutua ambaye kwa wakati mmoja aliwahi kuwa gavana wa kaunti ya Machakos.

Read More
 RAPPER JULIANI NA LILIAN NG’ANG’A WAFUNGA NDOA YA KIMYA KIMYA

RAPPER JULIANI NA LILIAN NG’ANG’A WAFUNGA NDOA YA KIMYA KIMYA

Rapper Juliani ameripotiwa kufunga ndoa ya kimya kimya na mchumba wake Lilian Ng’ang’a  baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa muda. Kulingana na wajuzi mambo kwenye mitandao ya kijamii,Harusi hiyo ambayo inadaiwa kuwa ya siri imiefanyika jijini Nairobi na kuhudhuriwa na watu wachache wakiwemo wanafamilia pamoja na marafiki. Mashabiki wengi kwenye mitandao ya kijamiii wameonekana kufurahia hatua ya wawili hao kuhalalisha mahusiano yao huku wengine wakiwa na mshangao kwanini ndoa hiyo imekuwa ya siri. Hata hivyo Juliani na Lilian ng’ang’a hawajathibitisha chochote kuhusiana ndoa yao hiyo ila ni jambo la kusubiriwa. Uhusiano wa kimapenzi kati ya rrapa Juliani na Lilian Ng’ang’a ulianza mapema mwaka jana , huku Juliani akithibitisha mahusiano hayo rasmi baada ya ukaribu wake na mrembo huyo gumzo mtandaoni ambapo  wengi walishangazwa na hatua ya msanii huyo kutoka kimapenzi na Lilian Ng’ang’a ikizingatiwa alikuwa mke wa Gavana wa Machakos Alfred Mutua. Ikumbukwe Agosti 15 mwaka 2021 Gavana Mutua na aliyekuwa mke wake Lilian nganga walitumia mitandao yao ya kijamii kuweka wazi kwamba hawapo tena pamoja hii ni baada ya ndoa yao kuvunjika miezi miwili iliyopita.

Read More