LINEX AACHIA PROJECT YAKE – TATU ZA MJEDA
Mkali wa muziki Bongofleva Linex Mjeda ameachia rasmi EP yake mpya inayokwenda kwa jina la tatu za Mjeda. Tatu za Mjeda EP ina jumla ya ngoma tatu za moto na bonus track moja ambapo amewashirikisha wakali kama Darassa na Belle 9. EP hiyo ina nyimbo kama Sherehe,Sina cha kupoteza na Siwema na inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mtandao wa kukisikiliza na kupakua muziki wa Boomplay. Tatu za Mjeda ni EP ya kwanza kwa mtu mzima Linex tangu aanze safari yake ya muziki baada ya dunia nyingine ya mwaka wa 2020 iliyokuwa na jumla ya mikwaju 5 za moto.
Read More