Liverpool Yaongeza Ngome ya Ulinzi kwa Kumsajili Frimpong

Liverpool Yaongeza Ngome ya Ulinzi kwa Kumsajili Frimpong

Klabu ya Liverpool inatarajiwa kumtangaza rasmi beki wa kulia wa klabu ya Bayer Leverkusen, Jeremie Frimpong, ndani ya saa 24 zijazo baada ya mchezaji huyo kukamilisha vipimo vya afya. Frimpong, raia wa Uholanzi mwenye asili ya Ghana, anakuja kama mbadala wa Trent Alexander-Arnold ambaye tayari ametangaza kuondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu. Liverpool wanaripotiwa kulipa ada ya pauni £29.5 milioni, ambayo ni sehemu ya kipengele cha kuachiliwa kilichopo kwenye mkataba wake na Leverkusen. Frimpong alikuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Leverkusen chini ya kocha Xabi Alonso, akisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa Bundesliga bila kupoteza mchezo wowote msimu wa 2024/25. Ujio wake Anfield unatazamiwa kuimarisha safu ya ulinzi ya Liverpool kuelekea msimu mpya wa EPL.

Read More
 LIVERPOOL NA ARSENAL YATOKA SARE YA KUTOFUNGANA KWENYE MCHEZO WA CARABAO

LIVERPOOL NA ARSENAL YATOKA SARE YA KUTOFUNGANA KWENYE MCHEZO WA CARABAO

Liverpool imelazimishwa Suluhu tasa na Arsenal katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya kombe la Carabao uliopigwa katika dimba la Anfield Januari 13 mwaka 2022. Arsenal walilazimika kucheza pungufu katika muda mwingi wa mchezo huo baada ya kiungo Granit Xhaka kuonesha kadi nyekundu mapema kipindi cha kwanza Hata hivyo Liverpool wameshindwa kutumia Mwanya huo na kutoa sifa kwa mbinu za mwalimu Mikel Arteta. Timu hizo zitarudiana juma lijalo katika dimba la Emirates kuamua Mshindi atakayetinga fainali ya michuano hiyo. Mshindi atakutana na Chelsea katika fainali

Read More
 MCHEZO WA ARSENAL DHIDI YA LIVERPOOL YASOGEZWA KISA CORONA

MCHEZO WA ARSENAL DHIDI YA LIVERPOOL YASOGEZWA KISA CORONA

Mchezo wa nusu fainali ya Carabao Cup, kati ya Liverpool dhidi ya Arsenal umesogezwa mbele, sababu kubwa ikiwa ni maambukizi ya Virusi vya Corona. Mchezo huo uliokuwa upigwe kesho Alhamisi kwenye Uwanja wa Anfield sasa utapigwa Januari 13 kisha marudio ni Januari 20, mwaka wa 2022. Liverpool chini ya Kocha Jurgen Klopp iliomba mchezo huo kusogezwa mbele kutokana na msaidizi wa kocha huyo, Pep Lijnders na wachezaji wengike kadhaa kuoata maambukizi ya Virusi vya Corona.

Read More