Lizzo Atoa Onyo kwa Marafiki wa Mafanikio: ‘Si Kila Rafiki ni wa Kweli’

Lizzo Atoa Onyo kwa Marafiki wa Mafanikio: ‘Si Kila Rafiki ni wa Kweli’

Msanii maarufu wa muziki wa pop na R&B, Lizzo, amezua gumzo mitandaoni baada ya kutoa kauli yenye mashiko kuhusu msanii mwenzake ambaye alianza kumkaribia tu baada ya yeye kupata umaarufu mkubwa. Akizungumza na podcast moja nchini Marekani, Lizzo amesema kuwa mtu huyo walikuwa wakitumbuiza naye katika maonyesho madogo kabla hajapanda chati za mafanikio, lakini hakuwahi kuwa karibu naye hadi alipoanza kupata umaarufu mkubwa kimataifa. Licha ya Lizzo kutomtaja msanii huyo kwa jina, amesisitiza kuwa si rahisi tena kuamini kila mtu anayejiita rafiki. Kauli hiyo imefasiriwa kama vijembe kwa watu wanaojitokeza kwenye maisha ya wasanii baada ya kuona mafanikio yao, huku wakisahau walikotoka pamoja. Mashabiki wengi wamemuunga mkono kwa kauli hiyo, wakisema inagusa maisha ya watu wengi waliofanikiwa kwa bidii zao. Wengine wameliona kama onyo la wazi kwa watu wanaotaka kuingia katika maisha ya wengine kwa maslahi ya muda mfupi. Kwa sasa, Lizzo anaendelea na kazi zake za muziki huku akisisitiza dhamira yake ya kuwa na watu wa kweli katika maisha yake ya kibinafsi na kitaaluma.

Read More