Davido Atoa Sababu za Kutoshiriki Tamasha la London
Msanii maarufu wa muziki wa Afrobeats kutoka Nigeria, Davido, ametangaza kujiondoa rasmi katika tamasha kubwa la muziki lililopangwa kufanyika katika uwanja wa Tottenham Hotspur jijini London, ambalo lilitarajiwa kufanyika Julai 2025. Tamasha hilo lilikuwa linamjumuisha pamoja na wakali wa muziki kutoka Marekani, 50 Cent na Mary J. Blige. Kupitia taarifa aliyoitoa kwenye mitandao ya kijamii, Davido alieleza kuwa licha ya tamasha hilo kupata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa mashabiki pamoja na mafanikio katika mauzo ya tiketi, kulikuwepo na matatizo ya msingi katika maandalizi na uendeshaji wa tukio hilo Katika maelezo yake, Davido alionyesha kutoridhishwa na mchakato mzima wa maandalizi na kuonyesha kuwa uamuzi huu umetolewa baada ya mazungumzo yaliyoshindikana kati ya pande mbili, jambo lililomfanya asisitize kutoshiriki kwenye tamasha hilo. Uamuzi huo umewashtua mashabiki wengi waliokuwa na matarajio makubwa ya kumuona msanii huyo akitumbuiza sambamba na majina makubwa ya muziki wa kimataifa. Hadi sasa, waandaaji wa tamasha hilo hawajatoa tamko lolote rasmi kuhusu kujiondoa kwa Davido au hatua watakazochukua baada ya mabadiliko hayo.
Read More