ROSE MUHANDO AKANUSHA TUHUMA ZA KUTOKA KIMAPENZI NA LORD MUTAI

ROSE MUHANDO AKANUSHA TUHUMA ZA KUTOKA KIMAPENZI NA LORD MUTAI

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili kutoka nchini Tanzania Rose Muhando amejitenga na tuhuma za kutoka kimapenzi na mwanablogu mwenye utata nchini Lord Mutai. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Rose Muhando amekanusha madai hayo kwa kusema kwamba hayana msingi wowote ikizingatiwa kuwa hamfahamu kabisa Lord Mutai. Kauli Rose Muhando imekuja mara baada ya mtumiaji mmoja wa mtandao wa Twitter kwa jina la Bookten kudai kuwa hitmaker huyo wa ngoma ya  “Nibebe” aliwahi kutoka kimapenzi na mwanablogu maarufu wa Twitter nchini Kenya Lord Mutai huko mjini Thika kwenye moja ya Hoteli aliyokuwa akifanya kazi. Bookten alienda mbali zaidi na kusema kwamba alimfumania Lord Mutai akimsindikiza Rose Muhando hadi kwenye chumba kimoja cha hoteli hiyo ambapo walilala hadi asubuhi. Hata hivyo baada ya taarifa hiyo kuzua gumzo mitandaoni Lord Mutai aliibuka na kujitenga na madai hayo kwa kusema kuwa hajawahi kutoka kimapenzi  na Rose Muhando katika hoteli yoyote mjini Thika ambapo alienda mbali zaidi na kutishia kumfungulia mashtaka Bookten kwa hatua ya kumpaka tope.    

Read More
 ROSE MUHANDO ATUHUMIWA KUTOKA KIMAPENZI NA MWANABLOGU MAARUFU NCHINI KENYA LORD MUTAI

ROSE MUHANDO ATUHUMIWA KUTOKA KIMAPENZI NA MWANABLOGU MAARUFU NCHINI KENYA LORD MUTAI

Msanii mashuhuri wa nyimbo za injili nchini Tanzania rose Muhando ameusimamisha mtandao wa Twitter kwa Jina lake kukaa kwenye orodha ya ‘Topics’ ambazo zinazungumzwa zaidi kwenye mtandao huo nchini Kenya. Hii ni baada ya mtumiaji mmoja wa mtandao wa Twitter kwa jina la bookten kudai hitmaker huyo wa ngoma ya  “Nibebe” aliwahi kutoka kimapenzi na mwanablogu maarufu wa Twitter Lord Mutai. Kulingana na Bookten aliwahi kufanya kazi kama mpokea wageni katika eneo la burudani liitwalo Club Image mjini Thika na alimuona Lord mutai akimsindikiza rose muhando hadi kwenye chumba cha hoteli katika klabu hiyo. Booktena alienda mbali zaidi na kudai kuwa bwana mutai alilala na rose muhando kwenye chumba hicho hadi asubuhi akihoji kuwa walishiriki tendo la ndoa. Hata hivyo bwana mutai amejitenga na madai hayo akisema kuwa hajawahi kutoka kimapenzi  na rose Muhando katika hoteli yoyote mjini Thika. Mutai amesema mawakili wake kwa sasa wako kwenye harakati ya kufuatilia shutuma zilizoibuliwa dhidi yake na Bookten.

Read More