LOUI AWEKA REKODI BILLBOARD AFRIKA KUSINI

LOUI AWEKA REKODI BILLBOARD AFRIKA KUSINI

Msanii wa Bongofleva Loui anaendelea kufanya makubwa kupitia  chati kubwa za Billboard Afrika Kusini. Hitmaker huyo wa “Hennessy”  amefikia hatua hiyo baada ya wimbo wao na mwimbaji Musa Keys kutoka Afrika Kusini,  uitwao “Selema (Po Po)” kuendelea kusalia kwenye chati hiyo ukiwa nafasi ya 20 kwa nyimbo zinazofanya vizuri Afrika Kusini, wiki hii. Kwa mujibu wa chart data tz wimbo huo umekaa kwenye chart hizo za Billboard kwa jumla ya wiki 13 na ulifanikiwa kushika nafasi za juu. Utakumbuka, wimbo huo wa “Selema” pia umeshafikia kiwango cha mauzo ya PLATNUM kwa Afrika Kusini, hivyo unamfanya msanii Loui kuwa miongoni mwa wasanii wa Tanzania kufikia mafanikio hayo baada ya msanii Diamond Platnumz.

Read More
 LOUI APOKEZWA CHETI CHA PLAQUE NA RECORDING INDUSTRY OF SOUTH AFRICA

LOUI APOKEZWA CHETI CHA PLAQUE NA RECORDING INDUSTRY OF SOUTH AFRICA

Msanii kutoka Tanzania Loui ameweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kuwa na wimbo uliofikisha hadhi ya Platinum nchini Afrika Kusini. Rekodi hiyo imewekwa kupitia wimbo wa SELEMA alioshirikiana na Musa Keys ambaye ni msanii na mtayarishaji kutoka nchini Afrika Kusini. Kwenye mkutano na Waandishi wa habari, mwimbaji huyo ametuonesha Certificate ‘Plaque’ ambayo ametunukiwa na Recording Industry of South Africa (RISA) kwa mafanikio ya wimbo huo. Mafanikio ya wimbo huo sio tu kwenye vituo vya Redio na Televisheni nchini Afrika Kusini bali ni hadi kwenye majukwaa makubwa ya kununua na kupakua muziki mtandaoni kama Spotify ambapo una zaidi ya Streams million 3.

Read More