Mahakama yatupilia mbali kesi iliyowasilishwa na Luba Events dhidi ya msanii Eddy Kenzo
Mwimbaji kutoka nchini Uganda Eddy Kenzo ana kila sababu ya kutabasamu baada ya mahakama kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa na  Luba Events kumzuia kutumbuiza jijini Kampala. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kenzo amewataarifu mashabiki zake kuwa ameruhusiwa tena kutumbuiza jijini Kampala kufuatia kesi ya Luba Events kukosa ushahidi wa kutosha mahakamani. Kenzo ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani kwa ajili ya tuzo za Grammy aliwakilishwa mahakamani na mawakili wake Kabega Musa, pamoja na Faisal Balikurungi. Mnamo Novemba, Eddy Kenzo alipigwa marufuku kutumbuiza jijini Kampala baada ya promota Moses Lubuulwa wa Luba Events kumburuza mahakamani kwa kukiuka mkataba wa kuandaa tamasha la “Eddy Kenzo Festival” lililomalizika hivi karibuni. Luba alieleza kuwa Eddy Kenzo alimsaliti aliposhindwa kumhuisha kwenye mandalizi ya tamasha hilo licha ya kumlipa fedha za kufanya ziara za “Eddy Kenzo Festival” katika maeneo mbalimbali nchini Uganda ikiwemo Masaka, Bundibujo na maeneo mengine. Hata hivyo alifichua kwamba alipata hasara ya kiasi cha Kshs, million 27 alipoandaa Tamasha la Eddy Kenzo mwaka 2020 ambalo halikufanyika kwa sababu ya Covid 19.
Read More