Lulu Diva Akanusha Tuhuma za Kutelekezwa na Kevin, Ex wa Hamisa Mobetto

Lulu Diva Akanusha Tuhuma za Kutelekezwa na Kevin, Ex wa Hamisa Mobetto

Msanii wa Bongo Fleva, Lulu Diva, ameibuka na kufafanua kuhusu madai ya mitandaoni yanayodai kuwa ametekelezwa kimapenzi na mfanyabiashara wa Togo, Kevin Sowax, ambaye pia ni ex wa mwanamitindo Hamisa Mobetto. Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti, Lulu Diva alisema hajawahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Kevin, wala kusafiri kwenda China kama inavyodaiwa. Alisema taarifa hizo zimemshangaza kwani hazina ukweli wowote na ni kama hadithi anazosikia kuhusu maisha yake, ambazo hata yeye huzisikia kutoka kwa watu. “Yaani hii ndiyo ile hali ya kusikia habari zako ikiwa hata wewe huzijui. Nimesikia minong’ono mingi kuhusu kutelekezwa sijui China. Mimi sijawahi kusema Kevin ni mpenzi wangu, wala sijawahi kwenda China. Hakuna kitu kama hicho bwana,” alisema Lulu Diva. Kuhusu kuwahi kuonekana hadharani akiwa na Kevin, Lulu Diva alisema hawezi kukataa kuwa waliwahi kuonekana pamoja, lakini hilo halimaanishi walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi. “Sikatai kama nimeonekana na Kevin pamoja, lakini hiyo si sababu ya kuhusishwa moja kwa moja na uhusiano. Sitaki hata kulizungumzia hilo kwa undani. Cha kuelewa ni kwamba siwezi kutelekezwa,” alisema kwa msisitizo. Msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya ‘Kipenseli’, alisema angetamani mashabiki wake waelekeze nguvu kwenye kazi zake za sanaa badala ya kushiriki kusambaza taarifa zisizo na msingi. “Naombeni mniache niko bize na Kipenseli. Naombeni sapoti ya kazi yangu,” aliongeza. Kwa miezi ya hivi karibuni, Lulu Diva amekuwa akitajwa mara kwa mara kwenye tuhuma za kimapenzi mitandaoni, hasa baada ya ripoti kuibuka kwamba anahusiana na Kevin, miezi michache baada ya mfanyabiashara huyo kuachana rasmi na Hamisa Mobetto mnamo Aprili mwaka huu.

Read More
 LULU DIVA AFUNGUKA KUHUSU KUVUJA KWA VIDEO ZAKE ZA UTUPU

LULU DIVA AFUNGUKA KUHUSU KUVUJA KWA VIDEO ZAKE ZA UTUPU

Msanii wa Bongofleva, Lulu Diva kwa mara ya kwanza kabisa amefunguka kuhusu sakata la kuvujishwa kwa video zake za faragha kwenye mitandao ya kijamii. Lulu Diva amesema kwamba video hiyo ilivujishwa na aliyekuwa mwanaume wake ambaye kwa sasa anaishi nchini Uingereza. “Nilikuwa naongea naye kimapenzi kama mpenzi wangu, ni mtu ambaye nilikuwa huru naye kwa sababu niliona ni kama mtu mzima,” amesema na kuendelea. “Kama sasa hivi nimebaki kujiuguza, lakini kama mwanaume ambaye nilikuwa naongea naye kama mpenzi wangu, unajua unaweza ukawa huru naye na kujiachia kama umetoka kuoga, ukawa uko wapi, hivo. Hata sijui hizo video anazo ngapi. Sijajirekodi mimi, amenirekodi yeye,” alisema Lulu Diva.

Read More