Lydia Jazmine amaliza tofauti zake na Prodyuza Bushingtone

Lydia Jazmine amaliza tofauti zake na Prodyuza Bushingtone

Msanii kutoka nchini Uganda Lydia Jazmine ameweka kando tofauti zake na prodyuza Bushingtone baada ya kuwa na ugomvi wa muda mrefu. Kulingana na taarifa za ndani, Wawili hao wameonekana wakiwa studio wakiandaa kazi mpya pamoja. “Wameelewana na tayari wako studio wanafanya kazi pamoja katika project kadhaa,” chanzo kimoja kimefichua. Jitihada za vyombo vya habari nchini Uganda kubaini ukweli wa taarifa hiyo hazikuzaa matunda ila ni jambo la kusubiriwa kutoka kwa duo zilikuwa bure kwa wakati wa vyombo vya habari. Utakumbuka mwaka 2010, Lydia Jazmine alitoka kimuziki kwa msaada wa Producer Bushingtone. Wawili hao walifanya kazi pamoja kwa muda hadi pale Lydia alipolamba dili nono la kutumbuiza katika mashindano ya Coke Studio nchini Kenya. Lakini wawili hao walikuja wakachanganya mapenzi na kazi kiasi cha kukosana vibaya, hivyo Lydia Jazmine akasajiliwa na mameneja kama R. Kampala, Ronnie Mulindwa na Mpaka Records ya Ykee Benda.

Read More
 Mwanamuziki kutoka Uganda Lydia Jazmine afunguka kupotea kimuziki

Mwanamuziki kutoka Uganda Lydia Jazmine afunguka kupotea kimuziki

Msanii wa kike kutoka nchini Uganda Lydia Jazmine amefunguka sababu za kutofanya vizuri kimuziki mwaka 2022. Kwenye mahojano yake hivi karibuni amesema aliamua kuweka kila kitu pembeni kwa ajili ya kujitathmini na pia amekuwa akiendeleza biashara zake kimya kimya. Mrembo huyo pia amedai kwamba mgogoro ulioibuka kati yake na uongozi  wake wa zamani ulilemaza juhudi za kuupambania muziki wake. Hata hivyo amesema mwaka 2023 anarudi na kishindo kwenye muziki wake kwani ana mpango wa kuachia nyimbo mfululizo bila kupoa. Utakumbuka Lydia Jazmine alivunja mkataba na meneja wake wa zamani Ronnie Mulindwa kutokana na migogoro ya kifedha lakini kwa sasa anafanya kazi kwa ukaribu na prodyuza Bushingtone.

Read More
 RONNIE MULINDWA ACHUKUA GARI ALIYOMZAWADI MSANII LYDIA JAZMINE

RONNIE MULINDWA ACHUKUA GARI ALIYOMZAWADI MSANII LYDIA JAZMINE

Meneja wa muziki nchini Uganda Ronnie Mulindwa ameripotiwa kuchukua gari aliyokuwa amempa aliyekuwa msanii wake Lydia Jazmine kipindi cha nyuma. Hii imekuja mara baada ya wawili hao kusitisha kufanya kazi pamoja kutokana na mzozo wa fedha. Ingawa jazmine awali alidai kuwa gari hilo lilinunuliwa kwa pesa zake lakini inaonekana hakuisajili akitumia jina lake. Juzi kati kwenye Birthday Party ya Nina Roz, Lydia Jazmine alisema tayari ameagiza gari lingine jipya ambayo ni nzuri ya mercedes benz ambayo meneja wake wa zamani alichukua kutoka kwake. Utakumbuka kwa sasa anafanya kazi na meneja wake wa zamani Bushingtone.

Read More
 LYDIA JAZMINE ACHUKIZWA NA UKOSEFU WA UMOJA MIONGONI MWA WASANII WA KIKE UGANDA

LYDIA JAZMINE ACHUKIZWA NA UKOSEFU WA UMOJA MIONGONI MWA WASANII WA KIKE UGANDA

Mwanamuziki Lydia Jazmine Jazmine amedai kuwa kuna mgawanyiko mkubwa katika biashara ya muziki, haswa miongoni mwa wasanii wa kike nchini Uganda. Akizungumza kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa Nina Roz, Jazmine amesema wasanii wakike wamekuwa wakionea wivu kimya hasa mmoja wao anapofanya vizuri kimuziki ambapo ameenda mbali na kudai muziki una nafasi kubwa ambayo inawatosha wasanii wote hivyo haoni umuhimu wa wasanii kutakiana mabaya. Msanii huyo amewataka wasanii wa kike nchini Uganda kuacha kutengeneza mazingira ya kugombana na badala yake washirikiane kwenye suala la kuipeleka mbele tasnia ya muziki nchini humo kimataifa. Hitmaker huyo wa ngoma ya “I Love you Bae” amesema atakuwa anahudhuria shughuli ya wasanii ambao ni wakweli huku akisusia ya watu ambao amewataja kama wanafiki Hata hivyo watu wengi wamehoji kuwa alikuwa anamrushia vijembe Spice Diana kwa kuwa hakuhudhuria hafla ya usikilizwaji wa albamu yake.

Read More
 LYDIA JAZMINE AFUNGUKA CHANZO CHA UKIMYA WAKE KWENYE MUZIKI

LYDIA JAZMINE AFUNGUKA CHANZO CHA UKIMYA WAKE KWENYE MUZIKI

Ni takribani miezi tano imepita kutoka staa wa muziki nchini uganda Lydia Jazmine aachie wimbo wake uitwao “Kapeesa” Ukimya wa  Lydia Jazmine  kwenye muziki umekuwa na maswali mengi sana kwa mashabiki na wadau wa muziki nchini Uganda. Sasa  kwenye mahojiano yake hivi karibuni Lydia Jazmine   ameweka wazi sababu zilizofanya akae kimya kwa miezi hiyo yote huku utaratibu wake wa kuachia nyimbo kwa miaka miwili ukiwa wa kusuasua. Lydia Jazmine ameweka wazi kuwa alikuwa anasumbuliwa na tatizo la  vidonda vya tumbo ulcers kwa zaidi ya miezi tano ila kwa sasa anamshukuru mungu amepona. Mrembo huyo ameweka wazi hilo alipokuwa anatambulisha wimbo wake mpya uitwao “Tonkoseza” ambapo amewataka mashabiki zake kukaa mkao kupokea nyimbo zake ambazo atakuwa anaachia back to back.  

Read More
 LYDIA JAZMINE ALALAMIKA KUTOPEWA HESHIMA KWENYE TASNIA YA MUZIKI NCHINI UGANDA

LYDIA JAZMINE ALALAMIKA KUTOPEWA HESHIMA KWENYE TASNIA YA MUZIKI NCHINI UGANDA

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Lydia Jazmine amesema kuwa kuna baadhi ya watu kwenye  tasnia ya muziki nchini humo hawatambui mchango wake. Hitmaker huyo wa “I Love Bae” amesema licha ya kuachia ngoma kali mwaka wa 2021 hajapewa heshima anayostahili kama wasanii wengine wakike nchini uganda. Mimi ni mmoja wa msanii ambao mwaka huu nimeachia ngoma 4 kali. Baadhi ya watu haoni na kutambua juhudi zangu lakini licha ya haayo yote upendi wenu mashabiki zangu ndio inanipa moyo wa kuendelea kufanya kazi.. Aliandika kupitia ukurasa wake wa Facebook. Hata hivyo hajabainika ni kitu gani kilipelekea mrembo huyo kutoa kauli hiyo ila wajuzi mambo kwenye mitandao ya kijamii wanahoji huenda hajafurahishwa na jinsi wasanii wapya wa kike nchini Uganda wanapokea upendo kuliko waliowatangulia. Ikumbukwe Lydia Jazmine hakushinda tuzo yeyote mwaka wa 2021 nchini Uganda licha ya kuachia ngoma kali kama Banange, Feeling, Kapeesa na nyingine nyingi. 

Read More