Mrembo wa Kenya Asema Hajakaa Chini kwa Wiki 5 Baada ya Kufanyiwa Upasuaji wa Kuongeza Makalio BBL
Mwanamitindo na mshawishi wa mitandao ya kijamii nchini Kenya, Lydia Wanjiru, amefichua kuwa hajakaa chini kwa zaidi ya wiki tano kufuatia upasuaji wa kuongeza makalio (BBL) alioufanyiwa hivi karibuni. Kupitia maelezo yake kwenye Instastory, Lydia amesema kuwa madaktari walimshauri kuepuka kukaa chini ili kutoleta madhara kwenye eneo lililotibiwa, hatua ambayo ni muhimu katika kipindi cha kwanza cha kupona. Mrembo huyo mwenye utata, amefafanua kuwa anaendelea kufuata maagizo hayo kwa uangalifu hadi atakapofikisha wiki sita, muda ambao ataruhusiwa kukaa kawaida bila kuhatarisha matokeo ya upasuaji wake. Hata hivyo amewashukuru mashabiki wake kwa ushirikiano na uvumilivu, akisema kuwa safari ya kupona imekuwa yenye changamoto lakini ana imani itakuwa na matokeo mazuri mara itakapokamilika.
Read More