Penzi la Pritty Vishy na Madini Classic laingiwa na ukungu

Penzi la Pritty Vishy na Madini Classic laingiwa na ukungu

Mrembo maarufu mtandaoni nchini Pritty Vishy amethibitisha kutokuwa na maelewano mazuri na mchumba wake msanii Madini Classic. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Mrembo huyo amesema kwa muda sasa hawajakuwa pamoja na Madini Classic kutokana na ugomvi ulioibuka kati yao juzi kati. Vishy amedai kwamba kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kutatua tofauti zao huku ukisisitiza kuwa ikitokea hawatapa mwarubaini wa ugomvi wao huenda wakavunja mahusiano yao rasmi. Kauli ya Pritty Vishy imepingwa vikali na Madini Classic ambaye amedai kuwa hawana tofauti zozote na mrembo huyo huku akikazia kuwa penzi lao lipo imara licha ya kutoonekana wakiwa pamoja katika siku za hivi karibuni.

Read More
 MADINI CLASSIC AWAJIBU WANAMKOSOA MPENZI WAKE PRITTY VISHY

MADINI CLASSIC AWAJIBU WANAMKOSOA MPENZI WAKE PRITTY VISHY

Msanii kutoka Mombasa Madini Classic amelazimika kumkingia kifua mpenzi wake mpya baada ya rafiki yake kudai kwamba ikiwa atamuoa Pritty, hatamzalia watoto wazuri. Kupitia ukurasa wake wa instagram, Madini amesema kuwa mchumba wake Pritty si kama wanawake wengi kwa sababu huwa Hariri picha anazoziweka kwenye mitandao yake ya kijamii. “Sielewi ni kwa nini wengi wenu mnafikiri Pritty si mrembo ni kwa sababu hachapishi picha zilizohaririwa mtandaoni kama baadhi yenu? Get to meet that chil physically utakubaliana nami that’s cute,” Madini aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram. Habari za wawili hao kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi zilianza kusambaa mapema mwezi uliopita, ambapo walikuja wakathibitisha kuwa ni wapenzi na hata wakaanza kusambaza picha zao wakiwa kwenye pozi za kimahaba zaidi kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii na blogu mbali mbali.

Read More
 MADINI CLASSIC AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA MWANAMKE ALIYEMZIDI KIUMRI

MADINI CLASSIC AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA MWANAMKE ALIYEMZIDI KIUMRI

Mwanamuziki Madini Classic amekanusha madai yaliyoibuliwa na walimwengu kuwa analelewa na mwanamke  huko Mombasa. Katika mahojiano na Nicholas Kioko, Madini amesema madai hayo hayana msingi wowote kwani yameibuliwa na baadhi ya watu ambao wanamwazia mabaya kutokana na mafanikio anayozidi kuyapata kupitia muziki wake. Hitmaker huyo wa “Bingi Bango” amewajibu wanaodai kuwa uhusiano wake na Pritty Vishy ni kiki kwa kusema kuwa hana muda wa kuwaaminisha watu kuwa anatoka kimapenzi  na mrembo huyo kwa kuwa masuala ya mahusiano ni ya watu wawili. Mbali na hayo amezungumzia ishu ya kuwaachumbia wanawake walioachwa na mastaa wenzake kwa kusema kwamba wanawake sampuli hiyo ni wapambanaji lakini pia wanajua sana mapenzi ikilinganishwa na wanawake wa watu wasiokuwa na umaarufu. Hata hivyo amewataka wakenya waache kumshambulia pamoja na mpenzi wake pritty vishy kwa kuwa penzi lao ni la kweli na hivi karibuni wana mpango wa kuhalalisha ndoa yao kwa njia ya harusi.

Read More
 PENZI LA PRITTY VISHY LAMKOSESHA USINGIZI MADINI CLASSIC.

PENZI LA PRITTY VISHY LAMKOSESHA USINGIZI MADINI CLASSIC.

Msanii Madini Classic amethibitisha kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Ex wa Stivo Simple Boy Prity Vishy ikiwa ni miezi kadhaa wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja. Katika mahojiano yake hivi karibuni Madini amesema alianza mahusiano yake kwenye mitandao ya kijamii alipomtumia ujumbe mfupi mrembo huyo na kumuomba namba ya simu huku akisema kwamba ujasiri na uhalisi wake ndio ilivutia sana. “I met her on Instagram, I texted her and asked for her mobile number. We started there. I like her courage and she’s real,” Amesema Madini. Hitmaker huyo wa ngoma ya Nilivyo amesema alipoweka wazi nia yake ya kutaka kumchumbia mrembo huyo, Vishy hakuamini na alisita kwa kuwa kipindi cha nyuma wasanii wengi wamekuwa wakimtafuta kwa ajili ya kufanya nae kazi. Madini Classic amewataka walimwengu kutomshambulia Vishy kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa inamuumiza kwa sana. “It really hurts me when I see people trolling her. She is an amazing personality when you get to interact with her and the trolls bring her energy down,” Amesema. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kutilia shaka madai ya Madini Classic na Pritty Vishy wakidai kuwa wana kazi ya pamoja wanafanya hivyo wanatumia suala hilo kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni. “Ati babe…ata haiendani. Hii clout haijaenda shule bado.”  Shabiki mmoja ameandika kwenye Instagram.  

Read More
 MADINI CLASSIC KWENYE PENZI JIPYA NA BABY MAMA WA MULAMWAH,CAROL SONNIE

MADINI CLASSIC KWENYE PENZI JIPYA NA BABY MAMA WA MULAMWAH,CAROL SONNIE

Msanii wa muziki nchini Madini Classic amethibitisha kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Carol Sonnie ambaye ni Baby Mama wa mchekeshaji maarufu  Mulamwah. Kupitia ukurasa wake wa Instagram msanii huyo ameweka wazi taarifa hiyo kwa mashabiki zake baada ya kuposti picha ya pamoja na mrembo huyo wakiwa kwenye pozi la kimahaba zaidi huku akiambatanisha na maneno yanayosomeka “Call me Mr. Polygamous. Wife number 2.”, akiashiri kuwa mrembo huyo amekubali kuwa mke wake wa pili. Ni kitendo ambacho kimeibua hisia mseto miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ambapo wengi wameonekana kumpongeza madini Classic kwa hatua ya kumpata mpenzi mpya huku wengine wakitilia shaka mahusiano yao kwa kusema kwamba huenda ni kiki ya kutangaza ngoma mpya ya Madini Classic. Utakumbuka Carol Sonnie na Baby Daddy wake Mulamwah walitangaza kuvunja mahusiano yao mwishoni mwa mwaka wa 2021 baada ya kukaa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa takriban miaka 5.

Read More