Rabadaba kutimuliwa nchini Uingereza kwa kukiuka sheria za uhamiaji
Sakata la ndoa ya msanii Rabadaba limechukua sura mpya baaada ya mke wake Maggie kutishia kutumia nguvu kumrejesha nchini kwao Uganda kwa kile alichokitaja kuwa mwanamuziki huyo alitumia njia ya magendo kuhamia nchini uingereeza. Kwenye sauti inayosambaa mtandaoni Mrembo huyo amesema Rabadaba hakuwa na upendo wa kweli kwake kwani lengo lake kuu ilikuwa kutumia ndoa yao kujipatia uraia wa nchi ya Uingereza bila kuzingatia sheria za uhamiaji. Aidha Maggie ambaye kipindi cha nyuma alikuwa kwenye mahusiano na marehemu AK47, amesema kwa sasa wakili wake ameanza kulifanyia kazi suala la kumhamisha Rabadaba nchini kwao Uganda kwa kuwa hatomvulia kwa jinsi alivyomsaliti kimapenzi. Utakumbuka mwaka 2021 Rabadaba na Maggie walihalalisha mahusiano yao kwa umma na kisha baadae wakahamia jijini London Uingereza ambako wanaishi kwa sasa lakini ndoa yao inasemekana imevunjika kwa madai ya usaliti.
Read More