Rapa Majirani afunguka sababu za kuacha kazi ya ujenzi katika nchini za miliki ya kiarabu

Rapa Majirani afunguka sababu za kuacha kazi ya ujenzi katika nchini za miliki ya kiarabu

Rapa Majirani amefunguka sababu kuacha kazi ya ujenzi aliyokuwa anafanya nchini Qatar na Saudia Arabia. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema aliamua kurejeni nchini kwa ajili ya matatizo ya kifya yaliyotokana na kuzidiwa athari ya viwango vya juu vya joto katika nchini za miliki ya kiarabu Hitmaker huyo wa “Tukumbukeko” amesema kwa sasa ana mpango wa kurejea shuleni kukamilisha masomo yake ya chuo kikuu, kuanzisha biashara na kukuza vipaji vya vijana mtaani kwao kupitia mchezo wa soka. Lakini pia amedokeza ujio wake mpya kimuziki kwa kuwataka mashabiki kukaa mkao wa kula kumpokea mwakani kwani anarudia kwa kishindo na muziki mzuri kwa lengo la kuirejesha jina lake kwenye ramani ya muziki kama alivyokuwa anafanya kipindi yupo nchini ya lebo ya muziki ya Grand pa Records. Hata hivyo Majirani amemamilizia kwa kuwataka wasanii waache kujificha kwenye maisha ya ustaa na badala yake wafanya shughuli zitakazowaingizia kipato kwa kuwa muziki haulipi kutokana na ukosefu mazingira mazuri ya kuwasaidia vijana kujiajiri kupitia muziki wao.

Read More
 MSANII WA ZAMANI WA GRANDPA RECORDS MAJIRANI AAPA KUTOFILISIKA TENA KIUCHUMI

MSANII WA ZAMANI WA GRANDPA RECORDS MAJIRANI AAPA KUTOFILISIKA TENA KIUCHUMI

Aliyekuwa msanii wa Grandpa Records Majirani amehapa kutofulia kiuchumi tena kutokana na masaibu aliyokumbana nayo kipindi cha nyuma. Msanii huyo ametoa ya moyoni kwa kusema kwamba umaskini ni kitu kibaya sana duniani huku akitupa kumbukumbu ya namna ambavyo mchumba wake alimkimbia licha ya kumtambulisha kwa wazazi wake kutokana na yeye kuyumba kiuchumi. Hitmaker huyo wa “Tukumbukeko” ameenda mbali zaidi na kusema kuwa kilichomuumiza zaidi na kitendo cha mchumba yake huyo kumnyima tendo la ndoa kwa kipindi cha miezi mitano. Utakumbuka mwaka 2021 majirani alijitokeza hadharani na kukiri kuwa anapitia wakati mgumu katika maisha yake ambapo aliwataka wakenya wamsaidie kifedha baada ya kufungiwa nyumba aliyokuwa akiishi kutokana na kushindwa kulipa kodi.

Read More