Malkia Karen Avishwa Pete ya Uchumba na Mpenzi Wake Zack

Malkia Karen Avishwa Pete ya Uchumba na Mpenzi Wake Zack

Mwanamuziki wa Bongofleva, Malkia Karen, ameanza ukurasa mpya maishani baada ya kuvalishwa pete ya uchumba na meneja wake, Zack, ambaye pia ni mpenzi wake wa muda mrefu. Tukio hilo limejiri baada ya miaka minane ya wawili hao kuwa kwenye mahusiano. Katika video iliyoenea mitandaoni, Zack alionekana akimpelekea Malkia Karen zawadi maalum ikiwemo pete ya uchumba, kadi yenye ujumbe wa mapenzi na simu mpya aina ya iPhone 17. Wakati wa tukio hilo, Malkia Karen alikuwa gym, akishuhudia hatua hiyo ya kipekee kutoka kwa mpenzi wake. Mashabiki wake wamefurahia tangazo hilo, wengi wakimpongeza kwa uvumilivu na safari ndefu ya mapenzi waliyoipitia na Zack. Tukio hili limeashiria mwanzo mpya wa maisha yao, huku ikitarajiwa sherehe kubwa ya harusi itakayofuata.

Read More
 MALKIA KAREN AKIRI KUACHA MUZIKI ASIPOSHINDA TUZO MWAKA HUU.

MALKIA KAREN AKIRI KUACHA MUZIKI ASIPOSHINDA TUZO MWAKA HUU.

Msanii wa Bongofleva, Malkia Kareen amesema mwaka huu asiposhinda tuzo kupitia wimbo wake mpya, Te Quiero ataacha muziki. Malkia Kareen amesema hayo kupitia XXL ya Clouds FM ambapo ameeleza wimbo huo anauona ukienda kufanya vizuri kwenye tasnia ya muziki Afrika Mashariki. “Nikikosa tuzo mwaka huu na huu wimbo naachana muziki,” amesema Malkia Karen. Utakumbuka Aprili mwaka 2021 Malkia Karen alifanikiwa kushinda tuzo mbili za Zikomo Awards kutoka nchini Zambia katika vipengele vya Best Female Artist Africa na Best Song of the Year kupitia wimbo wake, Sina.

Read More