JINAMIZI LAZIDI KUMUANDAMA TRAVIS SCOTT,MSANII WAKE AAHIDI KUFUNGUKA MAZITO

JINAMIZI LAZIDI KUMUANDAMA TRAVIS SCOTT,MSANII WAKE AAHIDI KUFUNGUKA MAZITO

Misala haiishi kwa Travis Scott, mwaka wa 2021 unakuwa mwaka mbaya kwake. Baada ya msala wa Astroworld sasa ni zamu ya msanii wake mpya Malu Trevejo Msanii huyo wa kike wa Travis anamshinikiza Rapa huyo kumuachia ajitoe kwenye uongozi wake kabla hajaanza kutoa ma-file yake mabaya Malutrevejo ameandika jumbe mbalimbali kupitia Instastory yake kwenye mtandao wa Instagram akimtaka rapa huyo kuvunja nae mkataba la sivyo ataanika madudu yote. Travis Scott alimsaini Malu Trevejo mapema mwaka huu baada ya kukiona kipaji chake kupitia mtandao wa TikTok. Miezi mitatu baadaye, Malu alitangaza kujitoa kwenye label hiyo (Cactus Jack) na Kutangaza kujiunga na Atlantic Records.

Read More