MWANAMUZIKI KUTOKA COLOMBIA MALUMA KUTUA AFRIKA HIVI KARIBUNI

MWANAMUZIKI KUTOKA COLOMBIA MALUMA KUTUA AFRIKA HIVI KARIBUNI

Tegemea ujio wa nyota mkubwa wa muziki wa kilatin kutoka taifa la Colombia Maluma ndani ya bara la Afrika katika siku za hivi karibuni. Maluma ambaye ametikisa dunia kwa mikwaju yake tofauti tofauti ikiwemo ngoma ya ” Mama Tetema” aliyoshirikiana na nyota wa muziki nchini Tanzania rayvanny., amethibitisha hilo kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram kwa kuandika ujumbe unaosomeka “See you soon Africa ” Hata hivyo safari ya mwanamuziki huyo kuja barani Afrika, huenda imechangiwa na mwanamuziki Rayvanny baada ya kuShare sehemu ya performance yake jijini Mbeya nchini Tanzania ambapo mashabiki walikuwa wakiimba na kulitaja jina la Maluma.

Read More
 RAYVANNY KUSHIRIKI KWENYE ZIARA YA MALUMA “PAPI JUANCHO” MWAKA WA 2022

RAYVANNY KUSHIRIKI KWENYE ZIARA YA MALUMA “PAPI JUANCHO” MWAKA WA 2022

Staa wa muziki kutoka nchini Tanzania, Raynvanny amehisiwa kuwa huwenda akashiriki ziara ya kimataifa ya nyota wa muziki wa nchini Colombia, Maluma. Rayvanny anahisiwa kuwa atashiriki ziara hiyo iliyopewa jina la album ya tano ya Maluma ‘Papi Juancho’ inayotarajiwa kuanza rasnu Februari 2021. Hii ni baada ya ujumbe wa Rayvanny kupitia ukurasa wake wa Instagram Disemba 14 2021 uliosomeka “SIJISIFII TOKA TUPATE UHURU HAUJAWAHI TOKEA WIMBO KAMA HUU EAST AFRICA PERIOD KAMA UNABISHA SEMA WEWE UPI ??? #MAMATETEMA GLOBAL WAY #CHUI @rayvanny @maluma MEET ME ON #PAPIJUANCHO TOUR ZOMBIE BABA @s2kizzy Maluma ameshatoa ratiba rasmi ya ziara hiyo ambapo itaanzia Zagreb Croatia, Februrari 24 na kumalizia April 10 huko Tel Aviv nchini Israel. Hii inafuata baada Rayvanny kuvunja rekodi ya kuwa Msanii wa kwanza kutokea Afrika kutoa burudani kwenye jukwaa la MTV EMA kwa mwaka 2021. Burudani hiyo ya kihistoria kwa tasnia ya muziki kwa msanii kutoka Afrika akiwakilisha Tanzania ilitolewa kwa wimbo wa Maluma,Mama tetema

Read More
 RAYVANNY ASHINDA TUZO UGANDA

RAYVANNY ASHINDA TUZO UGANDA

Mwanamuziki Rayvanny ameongeza tuzo katika kabati lake la tuzo baada ya kushinda tuzo ya Hipipo Music Award katika kipengele cha African Best Act 2021. Tuzo hizo kutoka Uganda zimemtaja Rayvanny kushinda tuzo kupitia wimbo wa Mama Tetema ambao ameshirikishwa na mwanamuziki kutoka Colombia Maluma, wimbo ambao ni Remix version ya wimbo wake wa Tetema. Wimbo huo uliachiwa rasmi Novemba 12 mwaka huu ambapo ulitambulishwa kwenye Jukwaa la Tuzo za MTV EMA na kumfanya Rayvanny kuwa msanii wa kwanza Barani Afrika kufikia hatua hiyo.

Read More