Chris Brown Aahidi Kurejea Kwa Kishindo Kwenye Breezy Bowl Tour

Chris Brown Aahidi Kurejea Kwa Kishindo Kwenye Breezy Bowl Tour

Mwanamuziki nyota kutoka Marekani, Chris Brown, amevunja ukimya kwa mara ya kwanza baada ya kuachiwa kwa dhamana mapema leo, akieleza kuwa yuko tayari kuendelea na ratiba ya onyesho lake kubwa la Breezy Bowl linalotarajiwa kuanza Juni 13 jijini Manchester, Uingereza. Kupitia ujumbe aliouweka kwenye mitandao ya kijamii, Chris Brown aliandika:  “Kutoka kifungoni mpaka kwenye Jukwaa la Breezy Bowl,” kauli iliyowasisimua mashabiki wake duniani kote. Taarifa za awali zilieleza kuwa msanii huyo alikumbwa na mkasa wa kuwekwa rumande kwa muda, hali iliyozua sintofahamu kuhusu mustakabali wa ziara yake ya kimuziki barani Ulaya. Hata hivyo, kwa mujibu wa ujumbe wake, Brown ameweka wazi kuwa yuko huru na amejipanga vilivyo kwa ajili ya tamasha hilo ambalo limekuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki. Chris Brown, anayefahamika kwa uwezo wake wa kipekee wa kuimba, kucheza na kutumbuiza jukwaani, anatarajiwa kufanya maonyesho katika miji kadhaa barani Ulaya kupitia ziara ya Breezy Bowl, ambayo ni sehemu ya kampeni ya kuendeleza album yake ya hivi karibuni na kusherehekea mafanikio yake ya kimuziki. Mashabiki nchini Uingereza na sehemu nyingine za dunia sasa wana kila sababu ya kuwa na matumaini kuwa tamasha hilo litaendelea kama ilivyopangwa, huku Chris Brown akiahidi kuwaletea burudani ya hali ya juu licha ya changamoto zilizojitokeza.

Read More
 Chris Brown Akamatwa Jijini Manchester kwa Tukio la Mwaka 2023

Chris Brown Akamatwa Jijini Manchester kwa Tukio la Mwaka 2023

Msanii nyota wa muziki wa R&B kutoka Marekani, Chris Brown, ameripotiwa kukamatwa jijini Manchester, Uingereza, muda mfupi baada ya kutua nchini humo kwa ndege binafsi (private jet). Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya usalama, maafisa wa Metropolitan Police (Met) walimkamata msanii huyo mara baada ya kubaini uwepo wake jijini humo. Kukamatwa kwake kunahusishwa na tukio la mwaka 2023, ambapo alidaiwa kumpiga kwa chupa ya mvinyo mtayarishaji wa muziki wa London aitwaye Abe Diaw, kitendo kilichosababisha majeraha makubwa hadi kusababisha kupoteza fahamu kwa muda. Chris Brown kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiano ya kina, huku uchunguzi ukiendelea kubaini mazingira kamili ya tukio hilo. Baada ya tukio hilo la mwaka jana, Abe Diaw alimfungulia Chris Brown kesi ya madai, akitaka alipwe fidia ya takribani dola milioni 16 za Marekani (zaidi ya shilingi bilioni 2.1 za Kenya), kwa madai ya majeraha ya kudumu, usumbufu wa kisaikolojia na kupoteza mapato kutokana na kushindwa kuendelea na kazi ya muziki kwa muda. Mpaka sasa, Chris Brown bado hajatoa taarifa rasmi kupitia timu yake ya mawakili wala mitandao yake ya kijamii kuhusu kukamatwa kwake. Hii si mara ya kwanza kwa Chris Brown kukumbwa na matatizo ya kisheria. Licha ya mafanikio makubwa katika muziki, amewahi kujikuta matatani mara kadhaa kutokana na matukio ya fujo au unyanyasaji. Tukio hili jipya linaongeza orodha ndefu ya changamoto za kisheria zinazomwandama nyota huyo.

Read More