Manchester City Kumnasa Kiungo Chipukizi wa Norway kwa Shilingi Bilioni 2
Klabu ya Manchester City ipo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa kiungo wa kati kutoka Norway, Sverre Halseth Nypan, kwa ada ya uhamisho inayokadiriwa kuwa Euro milioni 15, sawa na takribani Shilingi bilioni 2.1 za Kenya. Nypan, ambaye ana umri wa miaka 18, anatokea katika klabu ya Rosenborg BK ya Norway, ambako amecheza tangu mwaka 2022. Katika kipindi hicho, amehusika kwenye michezo 62 na kufunga mabao 14, akionyesha kiwango cha juu licha ya umri wake mdogo. Kinda huyo anatajwa kuwa mmoja wa vipaji bora zaidi barani Ulaya kwa sasa, na uwezo wake wa kusoma mchezo, kupiga pasi za mwisho, na kudhibiti kasi ya mchezo umevutia macho ya kocha Pep Guardiola. Manchester City wanapanga kumuingiza kijana huyo katika mpango wa muda mrefu wa kukuza vipaji, huku uwezekano wa kumtoa kwa mkopo ili kupata uzoefu wa ligi kubwa ukiwa bado wazi. Ingawa hakuna tangazo rasmi lililotolewa, taarifa kutoka kwa vyanzo vya karibu na klabu zote mbili zinaeleza kuwa mazungumzo yako katika hatua za mwisho, na usajili huo unaweza kutangazwa rasmi wakati wowote.
Read More