Meta Yafuta Akaunti ya Instagram ya Mwanaharakati wa Tanzania Mange Kimambi  

Meta Yafuta Akaunti ya Instagram ya Mwanaharakati wa Tanzania Mange Kimambi  

Kampuni ya Meta imefuta rasmi akaunti ya Instagram inayomilikiwa na mwanaharakati wa Marekani mwenye asili ya Tanzania na mkosoaji mkali wa serikali ya Rais Samia Suluhu, Mange Kimambi. Mange amedai kuwa alipoteza kabisa akaunti yake yenye wafuasi zaidi ya milioni 2.7 siku ya Jumatano, Desemba 3, akisema hakuna dalili za kurejeshwa. Aidha, ameeleza kuwa amepigwa marufuku kutumia WhatsApp, ambayo pia inamilikiwa na Meta, hatua anayoiita jaribio la kumzuia kufikisha ujumbe kwa hadhira yake. Wakati uo huo, mwanaharakati mwingine ambaye ni mkosoaji wa serikali, Maria Sarungi, ameripoti kuwa akaunti yake ya Instagram imekuwa ikikumbwa na shadow ban, hali inayosababisha wafuasi wake nchini Tanzania kushindwa kuona maudhui anayochapisha. Mange na Sarungi wamekuwa miongoni mwa sauti zenye ushawishi mkubwa mtandaoni zinazokosoa kwa ukali utawala wa Rais Samia Suluhu, na hatua hizi kutoka Meta zimeibua mjadala mpana kuhusu uhuru wa kujieleza na usalama wa wanaharakati katika majukwaa ya kidijitali.

Read More
 Mange Kimambi Awataka Watanzania Kususia Shows za Wasanii

Mange Kimambi Awataka Watanzania Kususia Shows za Wasanii

Mwanaharakati mwenye asili ya Tanzania Mange Kimambi ameibua gumzo kubwa mitandaoni baada ya kutoa wito mkali kwa Watanzania kutowarudisha wasanii kwenye umaarufu, akiwatuhumu kushirikiana na serikali kupuuza maumivu ya wananchi. Kupitia ujumbe mrefu aliouweka mtandaoni, Kimambi amesema kuwa baadhi ya wasanii waliosimama na serikali na kuhalalisha vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu hawapaswi kupewa nafasi ya kurudi kwenye nafasi zao za ushawishi katika jamii. Mwanablogu huyo aliyegeukia uanaharakati, amesema kwamba kurejesha umaarufu wao ni sawa na kuidhinisha uhalali serikali haramu na kudhoofisha kile anachokiita harakati za ukombozi. Kimambi, amedai kuwa wasanii wamekuwa wakitumia wananchi kwa miaka mingi kwa kuwafanya watumie pesa zao kuhudhuria shughuli, matamasha na maudhui yao mtandaoni, huku wakikosa kuzungumzia masuala mazito yanayowakabili wananchi. Hata hivyo ametoa pendekezo la kuanzishwa kwa kampeni ya ku-unfollow kurasa za mitandao zinazochapisha habari za umbea na kuwasukuma wasanii kwenye trending, akisema kuwa hatua hiyo itapunguza uwezekano wa wasanii kurejea kwenye nafasi ya ushawishi bila kuwajibika kwa yale yaliyopita.

Read More