Entertainment

Mange Kimambi Awataka Watanzania Kususia Shows za Wasanii

Mange Kimambi Awataka Watanzania Kususia Shows za Wasanii

Mwanaharakati mwenye asili ya Tanzania Mange Kimambi ameibua gumzo kubwa mitandaoni baada ya kutoa wito mkali kwa Watanzania kutowarudisha wasanii kwenye umaarufu, akiwatuhumu kushirikiana na serikali kupuuza maumivu ya wananchi.

Kupitia ujumbe mrefu aliouweka mtandaoni, Kimambi amesema kuwa baadhi ya wasanii waliosimama na serikali na kuhalalisha vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu hawapaswi kupewa nafasi ya kurudi kwenye nafasi zao za ushawishi katika jamii.

Mwanablogu huyo aliyegeukia uanaharakati, amesema kwamba kurejesha umaarufu wao ni sawa na kuidhinisha uhalali serikali haramu na kudhoofisha kile anachokiita harakati za ukombozi.

Kimambi, amedai kuwa wasanii wamekuwa wakitumia wananchi kwa miaka mingi kwa kuwafanya watumie pesa zao kuhudhuria shughuli, matamasha na maudhui yao mtandaoni, huku wakikosa kuzungumzia masuala mazito yanayowakabili wananchi.

Hata hivyo ametoa pendekezo la kuanzishwa kwa kampeni ya ku-unfollow kurasa za mitandao zinazochapisha habari za umbea na kuwasukuma wasanii kwenye trending, akisema kuwa hatua hiyo itapunguza uwezekano wa wasanii kurejea kwenye nafasi ya ushawishi bila kuwajibika kwa yale yaliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *