Mariah Carey aandika historia Spotify

Mariah Carey aandika historia Spotify

Wimbo wa Mariah Carey “All I Want for Christmas is You” umekuwa wimbo namba moja duniani baada ya kuvunja rekodi ya Spotify kwa kuwa na streams nyingi ndani ya saa 24. Ngoma hiyo imefanikiwa kufikisha streams zaidi ya milioni 21 siku ya krismasi kwa saa 24 tu Sanjari na hilo Mariah Carey pia anaendelea kuvuna mabilioni ya fedha kupitia wimbo wake huo uliotoka mwaka 1994 ambapo kila mwisho wa mwaka kuelekea krismasi hujichukulia tena umaarufu duniani kote. Kwa mujibu wa ripoti ya Economist, kila mwaka humuingizia Mariah Carey fedha za mirabaha dola milioni 2.5 ambayo ni zaidi ya shillingi millioni 307 za Kenya.

Read More
 Mariah Carey aweka rekodi Billboard Hot 100 kupitia “All I Want For Christmass is You”

Mariah Carey aweka rekodi Billboard Hot 100 kupitia “All I Want For Christmass is You”

Mwanamuziki kutoka Marekani Mariah Carey bado anaendelea kuweka rekodi mbali mbali kupitia wimbo wake wa “All I Want For Christmass is You” baada ya wimbo huo kukamata tena namba moja katika chati za Muziki za Billboard Hot 100 . Wimbo huo ambao hutumiwa sana unapofika msimu wa Christmass,kwa mara ya kwanza mwaka 2017 uliingia Top 10 ya chati hizo, 2018 ukafanikiwa kuingia Top 5 na kisha kwa mfululizo ukakamata nafasi ya kwanza mwaka 2019, 2020 ,2021 na 2022 katika msimu wa Christmass. “All I Want For Christmass is You” ambao ulitoka rasmi Oktoba mwaka 1994, uliandikwa na kutayarishwa na Mariah Carey pamoja na Walter Afanasieff. Kwa mujibu wa ripoti ya Economist, kila mwaka humuingizia Mariah Carey fedha za mirabaha Dola milioni 2.5 ambayo ni zaidi ya Shillingi millioni 307 za Kenya.

Read More
 NICK CANNON ATAMANI PENZI LA MARIAH CAREY

NICK CANNON ATAMANI PENZI LA MARIAH CAREY

Ni miaka 8 imepita tangu ndoa yao ivunjike lakini Nick Cannon bado analikumbuka penzi lake na Mariah Carey. Kwenye mahojiano na Podcast ya The Hottee Talk Show, Cannon amesema hatoweza kuwa na upendo tena kama aliowahi kuwa nao akiwa na Mariah Carey. Aidha ameongeza kwa kusema, anaweza kurudiana na Mariah Carey kama mambo yatakuwa kama yalivyokuwa. Wawili hao walifahamiana mwaka 2005 lakini walianza mahusiano mwaka 2008, mwaka ambao pia walifunga ndoa. Ndoa hiyo ilivunjika mwaka 2014 lakini kwa pamoja wana watoto wawili mapacha, Moroccan na Monroe wenye umri wa miaka 11.

Read More