Martha Mukisa atangaza kuachia EP yake mpya mwezi Desemba 2022

Martha Mukisa atangaza kuachia EP yake mpya mwezi Desemba 2022

Mwanamuziki anayekuja kwa kasi nchini Uganda Martha Mukisa ameweka wazi tarehe ambayo ataachia EP yake mpya inayokwenda kwa jina la Sisaaga. Hitmaker huyo wa “Sango” amethibitisha kwamba EP yake itaingia sokoni Desemba 9 mwaka huu ikiwa na jumla ya nyimbo saba za moto. Mukisa amemtaja Oman Rafiki na Liam Voice kama wasanii waliomsaidia kuandika nyimbo zinazopatikana kwenye EP hiyo huku maprodyuza Nessim, Ronnie, Bash killer, na Brian beats ambao wamehusika pakubwa kuiandaa EP hiyo. Mrembo huyo anaamini kuwa EP hiyo, itamsaidia kupenya kwenye soko la kimataifa kutoka na ubora wake. Sisaaga EP inaenda kuwa kazi ya kwanza kwa mtu mzima Martha Mukisa tangu aanze safari yake ya muziki miaka kadhaa iliyopita.

Read More
 MARTHA MUKISA ASHTAKIWA KWA WIZI WA WIMBO

MARTHA MUKISA ASHTAKIWA KWA WIZI WA WIMBO

Mwanamuziki Martha Mukisa ameingia kwenye headlines nchini Uganda mara baada ya kutuhumiwa kuiba wimbo wa wasanii wa kundi la VTS Boys. Kulingana na wasanii hao Martha Mukisa aliimba mashairi yote ya wimbo wao uitwao “Its You” na kisha akaubadilisha jina kuwa “Ntibula” bila ridhaa yao baada ya kuuziwa wimbo huo na Nick Mulla ambaye aliwaandikia wimbo wao wa “Its You.” Wasanii hao wamehoji kuwa Martha Mukisa anafahamu kabisa wimbo huo ni wao ila ameamua kupuuza kuhusu hakimiliki ya kazi hiyo. Hata hivyo Martha Mukisa hajajibu kuhusu tuhuma za kuiba wimbo wa kundi la VTS Boys ila wasanii hao wametishia kumchukulia hatua kali za kisheria iwapo hatakata kuwalipa miraba ya wimbo wao.

Read More
 MARTHA MUKISA AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU UGOMVI WAKE NA EDDY YAAWE

MARTHA MUKISA AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU UGOMVI WAKE NA EDDY YAAWE

Mwanamuziki chipukizi nchini uganda Martha Mukisa amevunja kimya chake juu ya ugomvi unaoendelea kati yake na Eddy Yaawe kuhusu umiliki wa wimbo wao uitwao “Neteze” Katika mahojiano na runinga moja nchini Uganda, mwimbaji huyo amefichua kwamba walikesha usiku kucha katika studio za Dream zinazomilikiwa na Eddy Yaawe wakirekodi wimbo wao mpya “Neteze”. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Busy” ameeleza kuwa walirekodi wimbo huo siku mbili mfululizo huku wakilala studio. “Nilienda nyumbani kwake Kireka kisha tukafunga safari hadi kwenye studio zake. Tulianza kurekodi na kulala huko na siku iliyofuata tulitofautiana sana kuhusu jina la wimbo,” alisema. Martha Mukisa amesema bado anamshukuru Eddy Yaawe kwa ushirikiano huo licha ya tofauti zilizojitokeza kutokana na hakimiliki ya wimbo huo. Utakumbuka wimbo wa “Neteze” ambao ulikuwa umepakiwa kwenye akaunti ya Youtube ya Martha Mukisa ulifutwa na Eddy Yawe kutokana na masuala ya hakimiliki baada ya kutoelewa na uongozi wa msanii huyo kuhusu ishu ya kugawa mirahaba.

Read More
 EDDY YAWE NA MARTHA MUKISA WAINGIA KWENYE UGOMVI KISA UMILIKI WA WIMBO WA “NETEZE”

EDDY YAWE NA MARTHA MUKISA WAINGIA KWENYE UGOMVI KISA UMILIKI WA WIMBO WA “NETEZE”

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Eddy Yawe ameingia kwenye ugomvi na msanii chipukizi nchini humo Martha Mukisa kuhusu umiliki wa wimbo wao uitwao “Neteze”. Hii ni baada ya Eddy Yawe kufuta wimbo huo kwenye akaunti ya youtube ya msanii Martha Mukisa kwa kigezo kuwa wimbo wa “Neteze” ni wake. Kulingana na Eddy Yawe yeye ni ndio mmiliki halisi wa wimbo huo kwani aligharamia pesa zote za kutayarisha audio pamoja na video Hata hivyo chanzo cha karibu na Martha Mukisa kinadai kuwa msanii hyuo anaamini kwamba atarejesha wimbo kwenye akaunti yake ya youtube wakati huu uongozi upo kwenye mazungumzo na Eddy Yawe kutafuta suluhu ya mgogoro ulioibuka katika yao. Utakumbuka kipindi cha nyuma Eddy Yawe walizozana na Carol Nantogo kuhusu umiliki wa wimbo wao uitwao Tukigale ambapo aliweza kumpokonya mrembo huyo hakimiliki zote za wimbo huo.

Read More
 EDDY KENZO AMWAGIA SIFA MARTHA MUKISA, ADAI ANAMPA MOYO WA KUWASAIDIA WASANII CHIPUKIZI NCHINI UGANDA

EDDY KENZO AMWAGIA SIFA MARTHA MUKISA, ADAI ANAMPA MOYO WA KUWASAIDIA WASANII CHIPUKIZI NCHINI UGANDA

Msanii nyota kutoka nchini Uganda Eddy Kenzo anataka kila aliye karibu yake afanikiwe, amehamua kumpa maua yake Martha Mukisa akiwa hai. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Weekend” kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni amemsifia Martha Mukisa kwa kusema kwamba anapenda jinsi anavyofikiri lakini pia ubunifu wake kwenye muziki. Eddy Kenzo amesema Martha Mukisa amemempa moyo wa kuwasaidia wasanii chipukizii nchini uganda kupitia lebo yake ya muziki ya Big Talent Entertaintment. Martha Mukisa amekuwa akisuasua kimuziki kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita lakini nyota yake ilikuja ikang’aa mwaka wa 2021 alipofanya wimbo wa pamoja na Eddy Kenzo uitwao Sango. Utakumbuka Eddy Kenzo na Martha Mukisa wana ukaribu sana jambo ambalo limewafanya walimwengu kwenye mitandao ya kijamii kuhoji kuwa ni wapenzi.

Read More