Msanii Marya Alazwa Hospitalini Baada ya Kiharusi, Aomba Msaada wa Kifedha

Msanii Marya Alazwa Hospitalini Baada ya Kiharusi, Aomba Msaada wa Kifedha

Msanii maarufu wa Kenya, Marya, anayekumbukwa kwa kibao chake maarufu Chokoza alichomshirikisha Avril, kwa sasa amelazwa hospitalini baada ya kupata kiharusi (stroke). Taarifa zilizotolewa na marafiki wake wa karibu, akiwemo msanii Avril, zinaeleza kuwa Marya amekuwa akiendelea kupokea matibabu hospitalini kwa muda, na anatarajiwa kuruhusiwa hivi karibuni. Hata hivyo, hali yake bado si nzuri kwani amepooza upande mmoja wa mwili wake, hivyo atahitaji huduma ya karibu ya nyumbani. Katika ujumbe wake, Avril alieleza kuwa Marya anahitaji msaada wa kifedha ili kuandaa mazingira salama na yenye huduma bora nyumbani. Msaada huo unahitajika kwa ununuzi wa vifaa maalum kama kitanda cha hospitali, kiti cha magurudumu, godoro maalum, na vifaa vingine vya matibabu. Avril pia alitoa wito kwa mashabiki na Wakenya kwa ujumla kuendelea kumuombea Marya ili apate nafuu na aweze kurejea katika hali yake ya kawaida. Marya aliwahi kuwa mmoja wa wasanii wakubwa nchini, akijizolea umaarufu kupitia Chokoza na nyimbo nyingine zilizowahi kutamba. Ingawa amekuwa kimya kwa muda mrefu katika tasnia ya muziki, mchango wake bado unakumbukwa na wengi. Kwa sasa, jamii ya wanamuziki, mashabiki na Wakenya kwa jumla wanahimizwa kuungana kwa moyo wa utu na mshikamano, ili kumpa Marya matumaini na msaada anaohitaji katika kipindi hiki kigumu. Kwa yeyote anayetaka kuchangia, mchango unaweza kutumwa kupitia nambari ya simu 0723 207 376 kwa jina la Lilian Miring’u.

Read More
 MARYA WA NGOMA YA CHOKOZA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU MAISHA YAKE YA NDANI

MARYA WA NGOMA YA CHOKOZA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU MAISHA YAKE YA NDANI

Hitmaker wa ngoma ya “Chokoza”, Msanii Marya amefunguka na kudai kuwa kuna kipindi alitaka kujitoa uhai akiwa ana ujazito wa mtoto wake wa kwanza. Katika mahojiano yake na Munga Eve, Marya amesema mawazo ya kutaka kujiua ilikuja baada ya kupatwa na msongo wa mawazo, uhusiano wake na baba wa mtoto wake ulipoanza kuyumba akiwa na mimba ya miezi mitano. Mrembo huyo amesema ilikuwa na wakati mgumu sana kudhibiti msongo wa mawazo aliyokuwa nayo kipindi hicho ila mwisho alifanikiwa kujitoa katika hali hiyo baada ya kuacha kila kitu na kuanza kujifikiria kwanza kama njia ya kujitibu. Mbali na hayo amesema anajuta kutumia vibaya pesa alizokuwa anaingiza kupitia muziki wake kipindi ambacho  alikuwa na jina kubwa kwenye tasnia ya muziki nchini. Utakumbuka Marya ambaye alikuwa chini lebo ya muziki ya Ogopa Deejays  alikuwa moja kati ya wasanii wakike waliosumbua sana kwenye chati mbali mbali za muziki nchini kupitia ngoma kama Sishiki Simu,Chokoza na nyingine nyingi.

Read More