Masauti atangaza kukamilika kwa EP yake mpya

Masauti atangaza kukamilika kwa EP yake mpya

Mwimbaji nyota wa muziki nchini, Masauti anaunza mwaka 2023 kwa kishindo. Hitmaker huyo wa Ipepete ametangaza ujio wa EP yake mpya ambayo ameipa jina la Time. Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema EP hiyo ambayo ina jumla ya nyimbo 8 za moto imekamilika kwa asilimia mia moja huku akiwataka mashabiki zake kukaa mkao wa kuipokea kazi hiyo. “#Timep It’s Done… I’m So Excited Can’t wait for you Guys to listen to these 8 amazing Bangers Ni moto”,Aliandika. Ikumbukwe mwaka wa 2020 ulikuwa mwaka mzuri kwa Masauti mara baada ya kuachia EP yake iitwayo 001, Ep ambayo imefikisha zaidi ya streams Millioni moja kwenye mtandao wa Boomplay.

Read More
 MASAUTI AKIRI KUPATA UGUMU KUFIKIA BAHATI

MASAUTI AKIRI KUPATA UGUMU KUFIKIA BAHATI

Hitmaker wa “Sing’oki”, msanii Masauti amekiri kupata ugumu kumfikia msanii mwenzake Bahati tangu kukamilika kwa uchaguzi mkuu Agosti 9 mwaka huu nchini Kenya. Masauti amedai Bahati hapokei simu wala hajibu jumbe zake kwenye mtandao wa Instagram, kitendo ambacho kinampa wasi wasi kuhusu hali ya mkali huyo wa ngoma ya “Adhiambo.” Kauli ya Masauti imekuja mara baada ya moja ya shabiki yake kwenye mtandao wa Instagram kumuuliza kama ana mpango wa kufanya kazi ya pamoja na Bahati. Utakumbuka Bahati amekuwa kimya tangu apoteze kiti cha ubunge eneo la Mathare kwenye uchaguzi ambao alidai kwamba ulikumbwa na udanganyifu mwingi.

Read More
 MASAUTI AKANUSHA TUHUMA ZA WIZI ZILIZOIBULIWA NA MWANAMKE MMOJA DHIDI YAKE MJINI MOMBASA

MASAUTI AKANUSHA TUHUMA ZA WIZI ZILIZOIBULIWA NA MWANAMKE MMOJA DHIDI YAKE MJINI MOMBASA

Staa wa muziki nchini Masauti amekanusha tuhuma za kumuibia nguo za ndani, simu na hela mwanamke mmoja, mjini Mombasa. Katika mahojiano yake hivi karibuni amesisitiza kuwa mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la Bianca alikuwa na lengo la kumharibia jina huku akiweka wazi kuwa alikuwa anashinikiza kuondoka na Masauti katika ukumbi huo wa Burudani. Kauli ya masauti imekuja mara baada ya kuandikisha taaarifa katika kituo cha polisi cha Nyali baada ya mwanamke mmoja aliyefahamika kama Bianca kudai kuwa msaani huyo alimwibia nguo za ndani (Chupi) simu na ksh 20,000 nje ya jumba moja la burudani eneo la Nyali. Kwa mujibu walioshuhudia tuki hilo Februari 13 mwaka huu eneo Nyali,Mwanadada huyo alionekana akitolewa kwa lazima na Masauti nje yagari alilokuwa ameegesha nje ya ukumbi huo wa burudani huku mwanamke huyo akisistiza kuwa alipoteza vitu hivyo kwenye gari hilo.

Read More
 MASAUTI AFUNGUKA KUFUKUZWA NA PROMOTA JUKWAANI MOMBASA

MASAUTI AFUNGUKA KUFUKUZWA NA PROMOTA JUKWAANI MOMBASA

Staa wa muziki nchini Masauti amevunja kimya chake baada ya kudaiwa kuwa alifukuzwa jukwaani kwenye tamasha la muziki lilofanyika Mombasa wikiendi iliyopita. Kupitia waraka aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa instagram Masauti amesema masaibu yake yalitokana na promota wa tamasha hilo huku akiwataka mashabiki kutomulaumu mbosso kwani hakuwa mhusika mkuu wa show hiyo. “Sijataka kuongelea issue ya show ya Mombasa lakini pia nimeona nivunje ukimya ili kuepuka unafki. Najua mashabiki zangu wanahofu kutaka kujua what exactly happened ndio singependelea mtu atumie jina langu kuelezea my side of the story. Nataka niwaombe tu kwanza tukio hili lilitokea lisitumike kumharibia rafiki yangu @mbosso_ jina wakati siye aliyeandaa show hii,” amesema Masauti Hitmaker huyo wa No Stress amesema kuna mwanadada ambaye alimkatiza akiwa jukwaani anatumbuiza jambo ambalo lilimlazimu Willy M Tuva kuingilia kati ndipo akapewa nafasi tena ya kutumbuiza. “Makosa yatupiwe waandalizi wa show hio mchwara tena sio wote ni dada mmoja tu ambaye singependa nimtaje jina😏Yeye ndo hakutaka kuheshimu kazi yangu na kunionyesha thamani kama msanii wa nyumbani. Lakini kama mpambanaji niliamua kueka kazi kwanza maana sipendi kueka hisia zangu mbele kwakua nina familia nyuma inayoniangalia mimi tu. Siku ile ya show walienda kinyume na mahitaji yangu kwenye rider lakini wala sikuvunjika moyo kwakua ni kijana ninayepambania sanaa yangu ili familia yangu ipate rizki😣Hakukua ata na usafiri wangu ili kufika sound check,” amesema Masauti . Hata hivyo amesema mapromota wa tamasha hilo hawakufadhili  usafiri wake kutoka na kwenda kwenye show licha ya kuwa na mkataba wa makubaliano. Baada ya kama nusu saa hivi, nikiendelea kuperfoem nikaona nyuma kuna mvutano unaendelea kati ya management yangu na watu kwenye stage. Yuleyule dada alitaka kunikatiza show katikati😒Vita hivo viliendelea kati yao na uongozi wangu ambao ulipinga hilo wazo lao la kusmamisha show katikati. Dj alismamisha show kwasababu yule dada alimtishia kutomlipa🤬 mvutano uliendelea akaja @mzaziwillytuva aliyeingilia kati na kukataa mziki ukatishwe namna hio. Aliungana nasi show ikaendelea. Nikaimba na mashabiki zangu hadi wakati wangu ukaisha ndo nikashuka kwenye stage,” ameeleza Masauti. Kauli ya masauti inakuja siku chache baada ya Nadia Mukami kufunguka namna ambavyo walidhulumiwa kwenye tamasha la muziki lilofanyika mjini mombasa wikiendi hii iliyopita.

Read More