Mash Mwana Amshauri Bahati Awe na Msimamo Katika Muziki Wake

Mash Mwana Amshauri Bahati Awe na Msimamo Katika Muziki Wake

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Kenya, Mash Mwana, amemkosoa msanii Bahati kwa kukosa msimamo katika muziki wake, akimtaka aelewe anachotaka kufanya badala ya kuchanganya muziki wa injili na ule wa dunia (secular). Kupitia Instastory yake, Mash Mwana amesema kuwa Bahati anapaswa kuamua iwapo anataka kuimba muziki wa injili au secular, badala ya kufanya vitendo vya kushtua umma kwa ajili ya kiki. Msanii huyo, amesema kuwa hata kama Bahati anamiliki studio au ana uwezo wa kufanya muziki aina yoyote, anapaswa kuwa na mwelekeo thabiti unaoendana na thamani ya jina lake kama msanii mkubwa nchini humo. Mash Mwana ameongeza kuwa Bahati ni msanii ambaye watu wengi waliokoka walipata msukumo kupitia nyimbo zake za injili, na hivyo anapaswa kukumbuka mahali Mungu alikomtua na kuendelea kutumia kipaji chake kwa utukufu wa Mungu badala ya kuibua utata kupitia maudhui yasiyo na maadili.

Read More
 Mash Mwana Amtaka Bahati Arudi Kwa Mungu na Kuacha Muziki wa Matusi

Mash Mwana Amtaka Bahati Arudi Kwa Mungu na Kuacha Muziki wa Matusi

Msanii wa muziki wa injili nchini Kenya, Mash Mwana, amemkosoa vikali mwanamuziki Bahati, akimtaka kuacha kutoa nyimbo zenye maudhui ya matusi na anasa, na badala yake kurejea kwa Mungu. Kupitia Instagram, Mash Mwana amesema amekuwa akifuatilia mwenendo wa Bahati kwa muda, na amehuzunishwa na jinsi msanii huyo aliyewahi kuhubiri injili sasa amegeukia muziki unaopingana na maadili. Amesema wasanii wa injili wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa, lakini vitendo vya Bahati vinawachanganya vijana na kudhoofisha taswira ya muziki wa Kikristo nchini. Kwa mujibu wa Mash Mwana, Bahati alikuwa nembo ya imani na uongozi wa kiroho katika muziki wa injili, lakini amepoteza mwelekeo kwa kuruhusu umaarufu na fedha kumtawala. Ameongeza kuwa anaamini bado kuna nafasi ya Bahati kutubu na kurejea katika huduma ya Mungu, kwani vipaji vyote vinatakiwa kumtukuza Muumba. Hata hivyo, Mash Mwana amesisitiza kuwa hana chuki binafsi na Bahati, bali anazungumza kama ndugu katika imani anayetamani kumwona akirudi katika njia ya Mungu na kutumia sauti yake kuinua roho za watu badala ya kuwapotosha.

Read More
 ALBUM YA MASH MWANA “MAAJABU” YAACHIWA RASMI KWENYE DIGITAL PLATFORMS ZOTE DUNIANI.

ALBUM YA MASH MWANA “MAAJABU” YAACHIWA RASMI KWENYE DIGITAL PLATFORMS ZOTE DUNIANI.

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Mash Mwana, ameachia rasmi album yake mpya iitwayo “Maajabu the album”. Album hiyo ina jumla ya mikwaju 12 ya moto huku ikiwa na kolabo 8 kutoka kwa wakali kama Irene Robert, Daddy Owen, Guardian Angel, Levixone,Walter Chilambo,Mr Seed, Jabidii, Didi Man,na Boss MOG. “Maajabu the album ina nyimbo kama Zungusha, Moto, Never, Nowa,Fanya Njia na tayari inapatikana kwenye mitandao yote ya ku-stream muziki duniani. Maajabu ni album ya kwanza kwa mtu mzima Mash Mwana tangu aanze safari yake ya muziki mwaka wa 2015.

Read More
 MASH MWANA ATAJA JINA LA ALBUM YAKE MPYA

MASH MWANA ATAJA JINA LA ALBUM YAKE MPYA

Mwanamuziki wa Nyimbo za injili nchini Mash mwana ameweka wazi jina la album yake mpya atakayoiachia mwezi Julai  mwaka huu. Katika mahojiano na Spm buzz mash mwana amesema album yake mpya itaitwa “Maajabu the album” na uzinduzi wake utafanyika julai 10 Nairobi Cinema. Licha ya kutoweka wazi idadi ya ngoma zitakazopatikana kwenye album yake ya Maajabu, mash mwana ametusanua kuwa amewashirikisha wasanii kama Daddy Owen, Irene Robert, Walter Chilambo, Guadian Angel na wengine wengi kusikika kwenye album hiyo. Maajabu ni album ya kwanza kwa mtu mzima Mash Mwana tangu aanze safari yake ya muziki mwaka wa 2015.

Read More
 MASH MWANA ATHIBITISHA KUKAMILIKA KWA ALBUM YAKE MPYA

MASH MWANA ATHIBITISHA KUKAMILIKA KWA ALBUM YAKE MPYA

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Mash Mwana anaendelea kutupasha mapya kuhusu Album yake mpya ambayo ana mpango wa kuachia hivi karibuni. Mkali huyo wa ngoma ya “Nifungue” ametusanua kwamba Album yake mpya imekamilika na itaingia rasmi sokoni Julai 10 mwaka huu. Licha ya kutoweka wazi jina na nyimbo zitakazopatikana kwenye album yake hiyo Mash Mwana amewaomba mashabiki zake kukaa mkao wa kula kuipokea projeect hiyo. Hii itakuwa ni album ya kwanza kwa mtu mzima Mash Mwana tangu aanze safari yake ya muziki miaka 7 iliyopita.

Read More
 MASH MWANA AKANUSHA KULELEWA NA MWANAWAKE

MASH MWANA AKANUSHA KULELEWA NA MWANAWAKE

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Mash Mwana amekanusha tuhuma zinazotembea kwenye mitandao ya kijamii kwamba amekuwa akilelewa na mwanamke. Katika mahojiano yake hivi karibuni Mash Mwana amesema anawashangaa watu wanavyomsema vibaya mitandaoni kuwa kuna mwanamke anafadhili maisha yake ya kifahari huku akisisitiza kuwa vitu vyote vya kifahari anavyovimiliki ni kutokana na bidii yake. Hitmaker huyo wa ngoma “Nifungue” amesema wanaoneza uvumi huo mtandaoni wana chuki na mafanikio yake huku akiongeza kuwa kulelewa na mwanamke ni ulimbukeni uliopitiliza hivyo hawezi kufanya vitu kama hivyo. Kauli yake imekuja mara baada ya watu kudai kuwa gari aina Mercediz Benz aliyozawadiwa kwenye kumbukizi ya kuzaliwa kwake alipewa na mwanamke ambaye amekuwa akimlea kwa muda mrefu.

Read More