Mwimbaji wa nyimbo za injili Master Piece awajibu wanaoponda muziki wake

Mwimbaji wa nyimbo za injili Master Piece awajibu wanaoponda muziki wake

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Master Piece amejibu wanaodai kuwa ameacha muziki wa injili kimya kimya na kugeukia uimbaji nyimbo za kiduani kwa lengo la kujitafutia pesa. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Master Piece amewataka walimwengu waache tabia ya kuwakosoa wasanii na badala yake wasapoti muziki mzuri wanaoufanya kama njia ya kutangaza muziki wa Kenya kimataifa. Msanii huyo amesema kuimba nyimbo za mapenzi sio dhambi kama watu wengi wanavyodhani na kusisitiza kuwa ni suala ambalo lipo kwenye maandiko matakatifu, hivyo haoni umuhimu wa watu kutilia shaka uimbaji wake kwa kuwa bado anamtumikia Mungu. Katika hatua nyingine Master Piece amemtolea uvivu msanii Willy Paul kwa kusema kwamba msanii huyo aliishusha brand yake ya muziki alipoamua kununua gari aina ya matatu kwani haeindani na kiwango cha maisha anayoishi kwa sasa. Hata hivyo amezungumzia suala la kutaka kumpeleka kanisani Mrembo Huddah Monroe kwa kusema kuwa hakuwa na nia ya kumchumbia mrembo huyo kimahaba bali alitaka kumtumia kubadilisha maisha ya vijana wengi kupitia umaarufu alionao kwa jamii ili waweze kukumbatia uwokovu.

Read More
 MASTERPIECE AMCHANA KIMTINDO WILLY PAUL KISA KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA MATATU

MASTERPIECE AMCHANA KIMTINDO WILLY PAUL KISA KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA MATATU

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Master Piece ameamua kufufua bifu yake na Bosi wa Saldido baada ya kuonekana kuponda hatua ya Willy Paul kuwekeza kwenye sekta ya matatu. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Masterpiece ameandika “Naskia kuna mtu amenunua mat ya ronga”, ujumbe ambao umetafsiriwa ni vijembe kwa Willy Paul ambaye juzi kati alitangaza kununua matatu. Sasa posti yake hiyo imeonekana kuwakera watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao wamemshushia kila aina matusi masterpiece wakidai kuwa muziki umemshinda ndio maana amegeukia maisha ya kulelewa na mwanamke anayemzidi kiumri. Hata hivyo wameenda mbali na kumtaka msanii huyo afurahie mafanikio ya wasanii wengine badala ya kudharau shughuli zao ambazo zinawaingizia kipato. Ikumbukwe Masterpiece na Willy Paul hajakuwa na maelewano mazuri kwa muda sasa, mwaka wa 2020 walirushiana maneno makali kwenye mitandao ya kijamii kisa uvaaji wa mavazi.

Read More