WILLY PAUL ATANGAZA KUWANIA UBUNGE MATHARE MWAKA 2022
Mwanamuziki nyota nchini Willy Paul ametia nia ya kugombea kiti cha ubunge eneo la Mathare kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022. Hitmaker huyo “My Woman” ameweka wazi hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwwa kuandika ujumbe unaosomeka “Are you ready Mathare? Lets bring that change #Levels, ujumbe unaowataka wakaazi wa Mathare kumuunga mkono kwenye azma yake ya kuleta mabadiliko katika eneo hilo. Willy Paul hajaweka wazi kama atawania wadhfa huo kama mgombea huru ama atatumia chamaa cha kisiasa kufanikisha azma yake hiyo ila ni jambo la kusbiriwa. Tangazo hilo la Willy Paul limeibua hisia mbali mbali miongoni mwa wakenya kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi wameonekana kutilia shaka uwezo wa Willy Paul kujiunga na siasa huku wengine wakiwataka msanii huyo ajitenge na siasa na badala yake awekeze nguvu zake kwenye kutoa muziki mzuri. Iwapo Willy Paul atafanikisha mpango wake wa kuwania ubunge wa Mathare mwaka wa 2022 atajiunga na wasani wenzake kama Rufftone, Jalang’o, Frasha, Gabu, na Prezzo.
Read More