Maua Sama mbioni kuachia Album mpya

Maua Sama mbioni kuachia Album mpya

Mwanamuziki wa Bongofleva Maua Sama anaunza mwaka 2023 kwa kishindo. kupitia ukurasa wake wa Instagram ametangaza kuachia album mpya Februari 14, kwenye siku ya wapendao maarufu kama Valentines. Maua Sama ameipa album hiyo jina la Love Waves yaani “Mawimbi ya upendo”. ”Album title Love Waves! This Valentine’s 2023”, Aliandika. Hata hivyo bado hajaweka wazi idadi ya nyimbo na wasanii walioshirikishwa kwenye album hiyo.

Read More
 Mashabiki zangu wengi wanaume – Maua Sama

Mashabiki zangu wengi wanaume – Maua Sama

Msanii wa Bongo Fleva, Maua Sama amedai mashabiki wake wengi ni wanaume na ndio maana imekuwa vigumu kwake kudumu kwenye mahusiano. Hata hivyo, tangu amekuwa maarufu kupitia muziki, Maua Sama hajawahi kuweka wazi mahusiano yake licha ya kuandamwa na tetesi za hapa na pale. “Mashabiki zangu wengi wanaume, ndio maana maboyfriend hawakai, huko kwenu vipi mnavumiliana?,” Maua Sama ameandika Twitter. Kwa sasa Maua Sama anafanya vizuri na remix ya wimbo wa Mwana FA, Sio Kwa Ubaya

Read More

MAUA SAMA AMJIBU ZUCHU KIMTINDO

Mwanamuziki wa Bongofleva, Maua Sama amewataka wasanii wenzake kuacha kupeana shinikizo zisizo kuwa na msingi kwenye masuala ya muziki. Kupitia ukurasa wake wa twitter Hitmaker huyo wa “ZAI” ameandika ujumbe unaosomeka “Wasanii tupunguze mikwara tutauana kwa pressur” na kumalizia na emoji ya kicheko. Ujumbe huo wa Maua Sama umetafsiriwa na walimwengu kuwa ni vijembe kwenda kwa Zuchu ambaye alidai kuwa kwa uandishi wake anafaa kuwekwa kwenye ligi ya wasanii wa kiume maana kina dada atawaonea. Utakumbuka kwa sasa Maua Sama anaendelea kufanya vizuri na Extended Playlist (EP) yake iitwayo “CINEMA” yenye jumla ya nyimbo saba za moto ambazo amewashirikisha wasanii wawili, Alikiba na Jux.

Read More
 MAUA SAMA ATAMANI KUINGIA KWENYE NDOA

MAUA SAMA ATAMANI KUINGIA KWENYE NDOA

Huenda tukio la Harmonize kumvisha Kajala pete ya uchumba limemgusa pakubwa mwimbaji wa bongofleva maua sama akitamani kuwa kwenye mahusiano, kwani ametangaza kuwa yupo single. Maua ametumia neno “Jimbo Lipo Wazi” akiwa na maana kwamba hayupo kwenye mahusiano kama ambavyo ujumbe huo unavyomaanisha huko mitaani. Maua sama ameandika “JIMBO LIPO WAZI ” akiwa ameambatanisha na emoji ya pete pamoja na pilipili. Hata hivyo kwenye post hiyo ya maua sama upande wa comments, mashabiki wake wanaonekana kutokubaliana nae kwa hilo wakiamini yupo mwenye jimbo lake.

Read More
 MAUA SAMA AACHIA RASMI EP YAKE MPYA

MAUA SAMA AACHIA RASMI EP YAKE MPYA

Staa wa muziki wa Bongo Fleva Maua Sama ameachia rasmi album yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake. Hitmaker huyo  wa ngoma ya “Zai” amewabarki mashabiki zake na  “Cinema EP” ambayo ina jumla ya nyimbo 7 za moto, ikiwa na kolabo 2 pekee kutoka kwa wakali kama Ali Kiba na Jux. EP hiyo kwa sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya ku-stream muziki duniani  ina ngoma kama Nioneshe, Fallingi in Love,  Tomorow, Namwachia, Vimba, Nimeridhia, na Never Ever. Hii ni EP ya kwanza kwa mtu mzima Maua Sama, tangu aanze safari yake ya muziki mwaka wa 2015.

Read More
 MAUA SAMA AWAACHA MASHABIKI NJIA PANDA

MAUA SAMA AWAACHA MASHABIKI NJIA PANDA

Mwimbaji nyota wa muziki wa Bongofleva, msanii Maua Sama amewaacha njia panda mashabiki wake kufuatia kuchapisha ujumbe unaoshiria yupo mbioni kuachia EP au Minitape. Katika post yake kwenye mtandao wa Instagram Maua Sama ametangaza kutengeneza wimbo mrefu sana wenye dakika 23, verse 14 na chorus 5. Maua Sama ambaye anajiita Maua Kobe ameeleza katika hizo dakika 23 amekata dakika 7 na amepata video 4. Hata hivyo amesema kuna verse mbili ambazo zimefanywa na wasanii wa kiume na kwa upande wa Beat wamehusika wataarishaji wane huku akiwahakikishia mashabiki zake kuwa wimbo huo utakuwa Ni mzuri. “Nimeamua kutengeneza wimbo mmoja mrefu sana. Una dakika 23, verse 14, chorus 5. Verse 2 wamefanya kaka zangu, beat imetengenezwa na watayarishaji 4”. Ameeleza Maua. “Nimekata dakika 7 nimepata video 4, ni muziki mzuri sana! Niamini mimi” aliongeza mauasama. “Weka HESHIMA kwenye jina langu”.Ameandika kupitia instastory yake.

Read More