MAUNDA ZORRO KUZIKWA JUMAMOSI HUKO TOANGOMA, DAR ES SALAAM.
Mwili wa aliyekuwa Msanii wa Bongo Fleva Maunda Zahir Zorro unatarajiwa kuagwa na kuzikwa siku ya Jumamosi ya Aprili 16 huko Toangoma, Kigamboni, Jijini Dar Es Salaam. Baba mzazi wa marehemu, mzee Zorro amesema shughuli zote za msiba zitafanyika nyumbani kwake maweni,Kigamboni na Marehemu atazikwa kwa sheria za dini ya Kikristo. Maunda Zorro alifariki Usiku wa kuamkia Aprili 14 katika ajali ya barabarani ambapo gari lake liligongana Uso kwa uso na Lori la Mchanga. Maunda amewaacha watoto watatu na atakumbukwa kwa nyimbo mbalimbali alizoshiriki ikiwemo ‘Nataka niwe wako’ na Mapenzi ni ya wawili’.
Read More