Msanii wa Uganda Maurice Kirya kustaafu muziki mwaka 2023

Msanii wa Uganda Maurice Kirya kustaafu muziki mwaka 2023

Msanii mkongwe kwenye muziki kutoka nchini Uganda Maurice Kirya ametangaza mpango wa kustaafu muziki. Kupitia ukurasa wake wa Instagram amewashukuru mashabiki kwa upendo ambao wamemuonesha kwa kipindi cha miaka 22 ambacho amekuwa akifanya sanaa. Aidha amesema mwaka 2023 ndio utakuwa mwaka wa mwisho kwake kujihusisha na sanaa baada ya kukamiliasha ziara yake ya kimuziki jijini New York, London, Paris Rotterdam, Berlin, Dubai, Nairobi, Kigali na Kampala. Hata hivyo chanzo cha karibu na msanii huyo kimesema Kirya ameechukua maamuzi hayo kwa ajili kukaa karibu na familia lakini pia kukuza biashara yake jambo ambalo litakuwa ngumu kwake kujihusisha na muziki. Utakumbuka wasanii kadhaa Uganda akiwemo Peter Miles na Ragga Dee wanafanya muziki na biashara huku wakilea familia zao kwa wakati mmoja

Read More
 MAURICE KIRYA AWAPA SOMO WASANII WAMBEA NCHINI UGANDA.

MAURICE KIRYA AWAPA SOMO WASANII WAMBEA NCHINI UGANDA.

Mwanamuziki kutoka Uganda Maurice Kirya amewapa somo baadhi ya wasanii wakubwa ambao wamekuwa na tabia ya kuwachamba au kuwazungumzia vibaya wasanii wenzao wakiwa kwenye shughuli zao za kimuziki. Kupitia mitandao yake kijamii Kirya ambaye ameonekana kukerwa na vitendo hivyo amesema kuna baadhi ya wasanii wakubwa nchini uganda ambao hutumia muda wao mwingi kuwasegenya na kuwakatisha tamaa wasanii wenzao badala ya kwenda studio kuboresha kazi zao za muziki. “Some of the most talented artists I know in Uganda spend most of their time gossiping about other artists and how they think they are better than them, Instead of getting in the studio and putting their talent to work,” Ameandika kwenye mitandao yake ya kijamii. Msanii huyo amewataka wasanii wanaoendeleza kasumba ya kuwasimanga wasanii wenzao kukoma mara moja na badala yake waelekeze nguvu zao kwenye suala la kutoa muziki mzuri. “So this goes out to you talented artists, if you think you’re good, stop trying to discourage artists that are actually doing the work and putting it out there. They are brave, and they’re following their dreams,”  Ameongeza. Utakumbuka miezi kadhaa iliyopita Mwandishi wa nyimbo na prodyuza Nince Henry alijitokeza na kudai kuwa kuna baadhi ya wasanii nchini Uganda wanaojihusisha na vitendo vya ushirikina ili wabaki kwenye tasnia ya muziki kwa muda mrefu.

Read More
 MAURICE KIRYA ATANGAZA KUWANIA URAIS WA MUUNGANO WA WANAMUZIKI UGANDA

MAURICE KIRYA ATANGAZA KUWANIA URAIS WA MUUNGANO WA WANAMUZIKI UGANDA

Mwanamuziki kutoka nchini uganda Maurice Kirya ametia nia ya kugombea  wadhfa wa urais katika muungano wa wanamuziki nchini humo kwenye uchaguzi ambao utafanyika hivi karibuni. Kirya amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Facebook kwa kusema kwamba amepokea maombi mengi kutoka wasanii wenzake pamoja na mashabiki, kugombea urais wa muungano huo kutokana na uelewa mpana ambao ako nao juu ya tasnia ya muziki nchini uganda. Msanii huyo amesema ana vigezo vyote vya kuwa rais wa muungano wa wanamuziki nchini Uganda huku akisisitiza kuwa lengo lake kuu ni kuwaunganisha wasanii na kuboresha kiwanda cha muziki nchini uganda kutokana na ujuzi ambao ameupata kwenye muziki wake Kauli ya Maurice Kirya imekuja mara baada ya msanii bebe cool kumtaka kuungana na wasanii Cindy Sanyu, Daddy Andre, na King Saha ambao tayari ametangaza kuwania kinyanganyiro cha urais wa muungano wa wasanii nchini uganda kwenye uchaguzi utakaofanyika hivi karibuni.

Read More
 MAURICE KIRYA MBIONI KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

MAURICE KIRYA MBIONI KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

Nyota wa muziki nchini uganda Maurice Kirya ameweka wazi jina la album yake mpya ambayo ana mpango kuachia ndani ya mwaka huu. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Maurice Kirya amesema album hiyo ameipa jina la The Road to Kirya  na itaingia sokoni Mei 6 mwaka 2022. Msanii huyo Amesema amewekeza pesa nyingi kuiandaa album hiyo ambayo kwa mujibu wake ni moja kati ya album ghali kutayarishwa na msanii wa afrika kwani ina muziki wa kitofauti sana ambao ni wasanii wachache hufanya barani afrika. Hii itakuwa ni Album ya 6 kwa mtu mzima Maurice Kirya,  tangu aanze safari yake ya muziki na itangumzia changamoto alizokutana nazo kwenye muziki wake

Read More