Prodyuza Mavo On The Beat aachia rasmi Album yake mpya

Prodyuza Mavo On The Beat aachia rasmi Album yake mpya

Prodyuza maarufu wa muziki wa Gengetone nchini Mavo On The Beat ameachia rasmi album yake mpya inayokwenda kwa jina la “Unajifanya.” Unajifanya album imebeba jumla ya mikwaju 17 ya moto huku zote zikiwa ni kolabo pekee. Mavo On The Beat ambaye amekuwa kwenye tasnia ya muziki kwa takriban miaka 10 amewashirikisha wasanii mbali mbali kama Wyre, Daddy Andre, Jua cali, Naiboi, Masauti, Exray, Mejja, Breeder LW, Rekless, Okello Max, Ssaru, Trio Mio na wengine wengi. Album ya “”Unajifanya” ni album ya kwanza ya mtu mzima Mavo On The Beat tangu aanze safari yake ya muziki mwaka 2013 na inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mitandao yote ya kukisikiliza na kuuza muziki duniani kama vile Boomplay,Spotify na Apple Music.

Read More
 PRODYUZA WA MUZIKI NCHINI MAVO ON THE BEAT AMCHANA DJ PINYE KWA KUKOSOA MUZIKI WA GENGETONE

PRODYUZA WA MUZIKI NCHINI MAVO ON THE BEAT AMCHANA DJ PINYE KWA KUKOSOA MUZIKI WA GENGETONE

Prodyuza wa muziki nchini Mavo On The Beat DJ amemchana DJ mkongwe Pinye kwa kauli yake aliyotoa kuwa ni vigumu kupiga muziki wa Gengetone kwenye soko la Kimataifa kutokana na muziki huo kukosa ubora. Akipiga stori na Plug TV prodyuza huyo amemsuta vikali DJ Pinye kwa kauli yake hiyo kwa kusema kuwa muda wake umepita na hana usemi kwenye  muziki wa Kenya hivyo aache swala la kuwaingilia wasanii wa Kenya ambao wanatia bidii kwenye kazi zao. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao wa kijamii wameonekana kutofautiana kimawazo na Mavo On The Beat ambapo wamemtaka  prodyuza ajikite kwenye ishu ya kuwashauri wasanii wa gengetone watoe muziki mzuri badala ya kuimba muziki ambao hauna mashiko kwa jamii. Ikumbukwe juzi kati DJ Pinye kwenye mahojiano na Standard Media aliwapa wasanii wa Kenya changamoto kutoa nyimbo zenye ubora ambazo zitapigwa katika mataifa kama Nigeria, Afrika Kusini na mataifa mengine ambayo yanaongoza kimuziki duniani.

Read More