Msanii Parroty Aingia Kwenye Bifu Kali na Militan Baada ya Kunyoa Dreadlocks Zake Bila Ridhaa

Msanii Parroty Aingia Kwenye Bifu Kali na Militan Baada ya Kunyoa Dreadlocks Zake Bila Ridhaa

Msanii Parroty ameingia kwenye bifu kali na mwenzake Militan kufuatia tukio la kushangaza lililotokana na mzaha wa soka. Parroty, ambaye ni shabiki mkubwa wa Manchester United, awali alitania kuwa angenyoa dreadlocks zake endapo timu yake ingepoteza dhidi ya Tottenham. Baada ya United kufungwa 1-0, hali ilichukua mkondo mpya. Mzaha huo sasa umegeuka kuwa chanzo cha mgogoro mkubwa baada ya Militan kumvamia Parroty na kumnyoa dreadlocks zake bila idhini. Paroty, kupitia mitandao ya kijamii, alielezea hasira na kukerwa kwake na tukio hilo, akilitaja kama udhalilishaji wa hali ya juu. “Hii imevuka mpaka. Sio kila kitu ni mchezo. Sikutegemea nishambuliwe kwa sababu ya maneno ya mzaha,” alisema Paroty, akionya kuwa iwapo watakutana na Militan ana kwa ana, huenda mambo yakaenda kombo. Mashabiki wameingia kwenye malumbano, baadhi wakidai Parroty alipaswa kutimiza ahadi yake, huku wengine wakimtetea wakisema tukio hilo lilikiuka heshima na haki za mtu binafsi. Kwa sasa, Militan bado hajajibu hadharani, huku mvutano ukizidi kuongezeka na tasnia ya burudani ikisubiri kuona hatma ya bifu hilo linalozidi kushika kasi.

Read More
 Msanii Tipsy Gee Amshutumu Militan wa Mbogi Genje kwa Kukata Dreadlocks za Parroty kwa Mabavu

Msanii Tipsy Gee Amshutumu Militan wa Mbogi Genje kwa Kukata Dreadlocks za Parroty kwa Mabavu

Msanii wa muziki wa Arbantone, Tipsy Gee, amezua mjadala mkali mtandaoni baada ya kumkemea vikali Militan, mmoja wa wanachama wa kundi la rap maarufu Mbogi Genje, kwa kile alichokiita kitendo cha kumvamia yeye na rafiki yake, Parroty, na kumnyoa dreadlocks zake kwa nguvu bila ridhaa yake. Tukio hilo lilitokea baada ya Parroty awali kuahidi kukata rasta zake endapo timu yake ya Manchester United ingefungwa na Tottenham Hotspur. Hata hivyo, licha ya Tottenham kushinda mechi hiyo, Parroty alibadilisha msimamo wake na kuomba msamaha kwa mashabiki, akisema kuwa angeacha kuishabikia Manchester United badala ya kukata rasta zake. Kwa mujibu wa Tipsy Gee, Militan alichukua sheria mkononi kwa kumshambulia Parroty na kumkata nywele bila makubaliano, kitendo ambacho kimezua hasira na lawama kutoka kwa wafuasi wa Parroty na wapenzi wa muziki wa mtaa. Mashabiki wengi wamejitokeza mitandaoni kulaani tukio hilo, wakilitaja kama ukiukaji wa haki ya mtu binafsi na ukosefu wa heshima. Wengine wameitaka Mbogi Genje kutoa msimamo rasmi kuhusu tukio hilo, huku wengine wakitaka hatua za kisheria zichukuliwe. Hadi sasa, Militan hajatoa tamko lolote rasmi kuhusiana na madai hayo. Tukio hili linaendelea kuzua mjadala mpana kuhusu mipaka ya mizaha, ahadi za mashabiki wa soka, na heshima kwa maamuzi ya mtu binafsi.

Read More
 MBOGI GENJE WAWEKA WAZI SABABU ZA KUMUUNGA MKONO RAILA ODINGA

MBOGI GENJE WAWEKA WAZI SABABU ZA KUMUUNGA MKONO RAILA ODINGA

Kundi la Mbogi Genje limefunguka sababu za kumuunga mkono kiongozi wa mrengo wa kisiasa wa Azimio la Umoja kwenye uchaguzi wa Agosti 9 mwaka huu. Katika mahojiano yao na 2mbili wasaniii wa kundi hilo wamesema walitoa wimbo kwa ajili ya kumsifia Raila Odinga kwa sababu walifuata upepo wa kisiasa nchini ambao ulikuwa unazungumzia sana kiongozi huyo wa kisiasa. Aidha wamepongeza hatua ya Raila Odinga kuelekea mahakamani kupinga matokeo ya urais kwenye uchaguzi uliokamilika kwa kusema kwamba alifanya jambo la busara badala ya kuwachochea wafuasi wake kuzua vurugu. Kitu kingine ambacho Mbogi Genje wamekizungumzia ni kuhusu ishu ya kumtenga member mwenzao Guzman kwa kusema kwamba ameshikika kwenye majukumu mengine, hivyo hawajamtoa kwenye kundi lao kama jinsi watu wanavyozungumza mitandaoni. Utakumbuka Mbogi genje ni kundi la linaloundwa na wasanii watatu ambao ni Militan, Guzman na Smady.

Read More
 BIFU LA KRG THE DON NA KUNDI LA MBOGI GENJE LACHUKUA SURA MPYA

BIFU LA KRG THE DON NA KUNDI LA MBOGI GENJE LACHUKUA SURA MPYA

Inaonekana bifu ya Mbogi Genje na Krg The Don haitapoa hivi karibuni hii ni baada ya wasanii wa kundi hilo kuibuka na kumchana Krg The Don kutokana na kauli aliyotoa majuzi kuwa wasanii wa mbogi genje ni wasanii wa mashinani. Wakiwa kwenye moja ya Interview wasanii hao wakiongozwa na Militant wamesema Krg The Don aache kujipiga kifua kuwa ni msanii wa kimataifa wakati ana idadi ndogo ya wafuasi kwenye mitandao kustream muziki duniani huku wakisema kama kweli Krg The Don angekuwa na pesa angewalipa baada ya kufanya nao kolabo kupitia wimbo wa Zible. Wasanii hao wa Mbogi Genje wameenda mbali zaidi na kusema kuwa hawana muda wa kupishana na Krg The Don ila hawakufurahishwa na hatua ya msanii huyo kukiuka mkataba wa maelewano kuhusu umiliki wa wimbo wa Zible baada ya kupakia video ya wimbo huo kwenye Youtube channel yake bila ridhaa yao. Mapema wiki Krg The Don aliibuka na kuwachana wasanii Mbogi Genje kuwa hawakugharamia chochote kwenye mchakato wa kuandaa audio na video wa wimbo wa Zible,  hivyo hawana haki ya kudai umiliki wa wimbo huo. Hii ni baada ya mbogi genje kudai kuwa Krg The Don aliwasiliti baada ya kukiuka mkataba wa maelewano kuhusu umiliki wa wimbo wa Zible alipoahamua kupakia video wa wimbo huo kwenye channel yake ya youtube bila idhini yao

Read More
 KUNDI LA MBOGI GENJE LATHIBITISHA KUWA KIBIASHARA ZAIDI BAADA YA KUANIKA MKEKA UNAONESHA BEI YA KUFANYA COLLABO NA SHOWS

KUNDI LA MBOGI GENJE LATHIBITISHA KUWA KIBIASHARA ZAIDI BAADA YA KUANIKA MKEKA UNAONESHA BEI YA KUFANYA COLLABO NA SHOWS

Kundi la muziki wa Gengetone nchini Mbogi Genje limetangaza kuwa kibiashara zaidi mara baada ya kuanika mkeka Unaonesha kiwango cha pesa wanachotoza kwa watu wanaotaka kufanya nao kazi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram mbogi genje wamesema kwamba kwa kila msanii anayetaka kufanya kolabo nao atalazimika kuwalipa shillingi laki 3 za Kenya huku wakiwataka waandaji wa matamasha kuwalipa shillingi elfu 150 kwa ajili ya kuwashirikisha kwenye shows zao. Hata hivyo watumiaji wa mitandao ya kijamii wameonekana kuwapongeza kwa hatua ya kugeuza muziki wao kuwa biashara zaidi huku wengine wakionekana kuwabeza kwa kulipisha pesa nyingi kwa shows na kolabo wakati muziki wao hauna mashiko

Read More
 KRG THE DON AWATOLEA UVIVU WASANII WA MBOGI GENJE KWA KUDAI WIMBO WA ZIBLE NI WAO

KRG THE DON AWATOLEA UVIVU WASANII WA MBOGI GENJE KWA KUDAI WIMBO WA ZIBLE NI WAO

Mwanamuziki wa dancehall nchini KRG The Don amenyosha maelezo kuhusu umiliki wa wimbo wa Zible aliowashirisha wasanii wa kundi la Mbogi Genje baada ya kundi hilo kudai kuwa KRG aliiba ubunifu wao. Katika mahojiano yake hivi karibuni KRG The Don amesema wasanii wa Mbogi Genje hawakugharamia chochote kwenye mchakato wa kuandaa wimbo huo, hivyo hawana haki ya kudai mirabaha ya wimbo wa Zible. KRG The Don amewatolea uvivu wasanii wa Mbogi Genje kwa kutumia lugha isiyokuwa na mashiko kuwasilisha ujumbe kwa mashabiki, kitu ambacho amedai kuwa imekuwa kizingiti kwa muziki wao kusikilizwa na watu wa umri wote katika jamii. Hitmaker huyo wa “Full kishunzi” amepuzilia mbali madai ya wasanii wa Mbogi Genje kuwa walimuandikia wimbo wa zible kwa kusema kwamba madai hayo hayana msingi wowote kwani alihusika pakubwa kuandika wimbo huo bila usaidizi wa mtu yeyote. Kauli ya KRG The Don imekuja mara baada ya wasanii wa kundi la mbogi genje kumtuhumu kuwa alishindwa kuwalipa alipowashirikisha kwenye wimbo wake uitwao Zible ambapo walienda mbali zaidi na kusema kwamba wao ndio walihusika kwa asilimia moja kwenye uandishi wa wimbo huo.

Read More