Album ya Mbuzi gang yafikisha streams zaidi ya milioni 1 Boomplay

Album ya Mbuzi gang yafikisha streams zaidi ya milioni 1 Boomplay

Album ya kundi la muziki nchini, Mbuzi Gang “Three Wise Goats” inaendelea kubadilisha namba kila leo kwenye digital platforms mbalimbali. Habari njema ni kwamba tayari imefikisha jumla ya Streams Milioni moja kwenye mtandao wa Boomplay ndani ya mwaka mmoja tangu itoke rasmi. Album hiyo ambayo ina jumla ya nyimbo 13 za moto,iliachiwa rasmi mwezi Januari mwaka 2022 ikiwa na kolabo 10 pekee kutoka kwa wakali kama Jose Chameleone, Lava Lava,KRG The Don, Nina Roz, Katapilla, Ethic, Madini Classic, Naiboi na wengine kibao. Kupitia ukurasa wao wa Instagram Mbuzi Gang wamewashukuru mashabiki zao kwa upendo kwa kuandika, “1 million Streams on this masterpiece. Thank you fam. #3WG” Ikumbukwe “Three Wise Goats” ni Album ya kwanza kwa kundi la Mbuzi Gang ambalo linaundwa na wasanii watatu ambao ni Fathermoh, Joefes na iphoolish.

Read More
 MBUZI GANG: KIBURI IMEWAPONZA WASANII WA GENGETONE

MBUZI GANG: KIBURI IMEWAPONZA WASANII WA GENGETONE

Wasanii wa kundi la Mbuzi Gang wamefunguka na kudai kwamba kiburi ndio imewaponza baadhi ya wasanii wa Gengetone. Katika mahojiano yao hivi karibuni wamesema baadhi ya wasanii wa muziki huo wameanza kulaza damu kutokana na kupata views nyingi kwenye mtandao wa youtube jambo ambalo limewapelekea kuingiwa na kiburi na kujiona ni wakubwa zaidi kuliko wasanii wenzao. Aidha wamepuzilia mbali madai kuwa muziki wa Gengetone umepitwa na wakati kwa kusema kuwa dhana hiyo imetokana na ukosefu wa ushirikiano miongoni mwa wasanii wa muziki huo. Katika hatua nyingine wamekanusha tuhuma zilizoibuliwa na baaadhi ya wasanii wa Gengetone kwamba lebo za muziki zinawanyanyasa huku wakisema kuwa wasanii hao ndio wakulaumiwa kwani wamekwenda kinyume na mikataba ya lebo wanazofanya kazi nazo kwa kutoachia nyimbo. Hata hivyo wamewataka wasanii wa Gengetone waache uvivu kwa kulalamika kuwa wanaporwa pesa zao na badala yake watie bidii kwenye shughuli zao za muziki ili waweze kupata riziki itakayowasaidia maishani.

Read More
 MBUZI GANG WAJIBU SUALA LA NYIMBO ZAO KUFANANA

MBUZI GANG WAJIBU SUALA LA NYIMBO ZAO KUFANANA

Wasanii wa kundi la Mbuzi Gang wamewajibu wale wanaosema kuwa nyimbo zao zinafanana. Katika mahojiano yao ya hivi karibuni wamesema madai hayo hayana ukweli wowote kwa kuwa wamekuwa wakiachia nyimbo zenye melodies tofauti zinazoenda na nyakati zilizopo. Wakali hao wa ngoma ya shamra shamra Wamesema wanaodai nyimbo zao zinafanana wanaowaona wivu kutokana na mafanikio ambayo wanayapata kwenye muziki wao huku wakisisitiza kuwa wataendelea kutoa muziki mzuri kwa ajili ya mashabiki zao. Kauli yao imekuja mara baada ya watu kudai kuwa tangu wapate umaarufu kupitia wimbo wao wa “Shamra Shamra” wamekuwa wakiachia nyimbo zenye melodies zinazofanana na wimbo huo.

Read More
 WASANII WA MBUZI GANG WAHUSIKA KWENYE AJALI YA BARABARANI

WASANII WA MBUZI GANG WAHUSIKA KWENYE AJALI YA BARABARANI

Msanii wa kundi la Mbuzi Gang, Fathermoh amethibitisha kuwa wasanii kundi hilo walihusika kwenye Ajali ya barabarani Februari 26. Fathermoh ameeleza hayo baada ya kuwepo na tetesi mitandaoni ambapo aliamua kuweka wazi suala hilo kupitia mtandao wa Instagram. Kwenye Insta Story yake msanii huyo ameandika kuwa ni kweli walipata Ajali lakini kwa sasa wapo salama ikizingatiwa kuwa hawakupata majeraha mabaya. Utakumbuka usiku wa kuamkia Februari 26 wasanii wa Mbuzi Gang walijaza nyomi la mashabiki katika ukumbi wa Alva Resort huko Maseno ambako walipiga show ya kufa mtu iliyowaacha mashabiki wakiwa na kiu ya kutaka burudani zaidi.

Read More
 WASANII WA KUNDI LA MBUZI GANG WAACHIA RASMI ALBUM YAO MPYA

WASANII WA KUNDI LA MBUZI GANG WAACHIA RASMI ALBUM YAO MPYA

Hatimaye wasanii wa kundi la muziki wa Gengetone nchini Mbuzi Gang wameachia rasmi album yao mpya iliyokuwa ikisubiriwa na mashabiki wao. Mbuzi Gang wamewabarki mashabiki zao na  “Three Wise Goats Album” , album ambayo ina jumla ya nyimbo 13 za moto, ikiwa na kolabo 10 pekee kutoka kwa wakali kama Jose Chameleone, Lava Lava,KRG The Don, Nina Roz,Katapilla, Ethic, Exray Taniua,Madini Classic, Naiboi na wengine kibao. Album hiyo kwa sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya ku-stream muziki duniani na ina ngoma kama Shida, Blessing, Goshodo, Rudi Nyumbani,Shifla, Zoza na nyingine nyingine. Hii  ni Album ya kwanza kwa kundi la Mbuzi Gang ambalo linaundwa na wasanii Fathermoh, Joefes na iphoolish

Read More